Video na Picha: HARUSI ISIYO NA GHARAMA YAZUA GUMZO..WAMETUMIA SHILINGI ELFU 2 TU..SHUHUDIA HAPA


Harusi isiyo na gharama,Wilson na Ann Wambui Kenya
Wanandoa wawili ambao taarifa yao ya harusi isiyo na gharama imezua gumzo na imevutia watu wengi katika mitandao ya kijamii na sasa watagharamiwa honeymoon (fungate) ya harusi hiyo.

Wilson mwenye umri wa miaka 26 na Ann Wambui mwenye umri wa miaka 24 alitumia shilingi za Kenya 100 sawa na shilingi 2,147 ya Tanzania,kununua pete mbili mbali na kuvaa tisheti za sherehe hiyo.

Hawakuwa na sherehe yoyote baadaye.

''Tulienda nyumbani, tukapika ugali na sukuma wiki tukala na kulala,hapakuwa na kitu chochote maalum ambapo tungefanya kama fungate yetu'', kulingana na eDaily News.

Kiongozi wa dini ambaye alihalalisha ndoa hiyo alisambaza habari yao katika mtandao wa facebook kabla ya kuchukuliwa na vyombo vya habari.

Mwakilishi wa kampuni ya Bonfire Adventure alikutana na wanandoa hao.

Harusi isiyo na gharama,Wilson na Ann Wambui Kenya
Wilson na Ann Wambui wakifunga ndoa
Harusi isiyo na gharama,Wilson na Ann Wambui Kenya
Wilson na Ann Wambui
Harusi isiyo na gharama,Wilson na Ann Wambui Kenya
TAZAMA HAPA CHINI VIDEO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527