SERIKALI YAPIGA MARUFUKU HARUSI ZA KIFAHARI ILI VIJANA WENGI WAOE


Mji mmoja nchini Somalia umepiga marufuku harusi za gharama ya juu ili kuwashinikiza vijana zaidi kuoa.

Kamishna wa wilaya Mohamud Hayd Osman wa Bula Hawa karibu na mpaka wa Kenya waliambia BBC kwamba ni mbuzi wasiozidi watatu ndio wanaofaa kuchinjwa pekee ili kuwalisha wageni na kwamba sherehe katika hoteli hazitaruhusiwa.

Amesema kuwa mahari itakuwa chini ya dola 150 pekee.

Uamuzi huo unajiri baada ya maafisa kubaini kwamba takriban watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa hivi karibuni.

Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio masuala yanayowafanya watu kulihama eneo hilo.

Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia.

"Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini, alisema Osman.

Hatua ya kupunguza matumizi kuhusu sherehe za kifahari pamoja na matumizi mengine baada ya ya maafisa kugundua kwamba ni kwa nini watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa mjini humo.

Wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha, alisema.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527