Picha 12: SHINDANO LA UREMBO KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI 'ALBINO' KENYA,MALKIA APATIKANA



Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.


Mamia walijitokeza kushuhudia maonyesho ya urembo ya Mr na Ms Albino nchini Kenya. Kila siku Albino wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na viungo vyao vya mwili kuuzwa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.
Malkia mpya! Louise Lihanda, aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada atembea jukwani akiwa amevalia vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa kutumia puto. Loiuse ambaye ni mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
Wanaume walioshiriki katika mashindano hayo wasimama  jukwaani. walishiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
Mfalme! Jairus Ongetta, ambaye amekabidhiwa taji ya uanamitindo bora kwa wanaume akiwa jukwaani na mavazi ya kupendeza.
Erick Thomas, awaongoza wanamitindo wenzake kwenye jukwaa wakati wa mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi. Lengo lake ni kuhakikisha kwamba watu walio na ulemavu huo wamejivunia ngozi yao.
Msichana huyu aliduwazwa na maonyesho hayo! Yeye ni miongoni mwa watu ambao kila siku wanakabiliwa na hatari ya kuuawa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.
Miraba minne! John Ngatia, ambaye pia huwa anasakata densi, avalia sare ya mapigano ya ndondi katika maonyesho hayo, jijini Nairobi Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
Majaji walikuwa macho! Waliongozwa na mwanamitindo wa kimataifa Deliah Ipupa (katikati) tarehe 21Oktoba 2016.
Naomi Wafula, ajitokeza jukwaani akiwa amevalia vazi lililotengenezwa kwa sahani za plastiki katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
Mamia walihudhuria maonyesho hayo kuonyesha umoja wao na watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi katika mgahawa wa Carnivore jijini Nairobi Kenya, tarehe 21, Oktoba 2016


Amina Makokha ajitokeza jukwaani akiwa amevalia sare ya mchezo wa raga katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
Kutoka kulia, naibu rais wa Kenya William Ruto, Mbunge Isaack Mwaura na mkurugenzi mkuu wa bodi ya filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua pia walikuwemo.

Chanzo-BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527