Makubwa Haya!! JAMAA AJICHINJA BAADA YA MPENZI WAKE KUCHUKULIWA NA MWANAMME MWINGINE DODOMA



Mwanamme aliyejichinja shingo akisaidiwa na wasamaria wema-Picha na Andrew Msafiri-Malunde1 blog Dodoma
 ******
 Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamme mmoja ambaye hajajulikana jina anayedaiwa kuwa ni mfanya biashara katika stendi ya mabasi ya Mpwapwa mkoani Dodoma amejichinja kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog limetokea leo Oktoba 25,2016 majira ya saa sita mchana baada ya jamaa huyo kukataliwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.

“Amejikata koromeo kwa kutumia kisu baada ya mwanamke aliyekuwa naye kumkataa kwa madai kuwa ana mwanamme mwingine,kitendo cha mpenzi wake kuchukuliwa na mwanamme mwingine ndicho kimemfanya achukue maamuzi hayo magumu ya kuondoa uhai wake”,mashuhuda wameiambia Malunde1 blog.

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo pamoja na mwanamme anayedaiwa kuchukua mpenzi wa mwanamme aliyejichinja pia wanafanya kazi katika stand hiyo ya mabasi.

Hata hivyo kutokana na kitendo hicho wasamaria walijitokeza kumsaidia mwanamme huyo na kumkimbiza katika hospitali ya wilaya ya Mpwapwa kwa ajili ya matibabu. 

Na Andrew Msafiri-Malunde1 blog Dodoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527