Kumekucha CHADEMA!! HUYU NDIYO KATIBU MKUU MPYA ATAKAYEVAA VIATU VYA DR SLAA



Dr. Vicent Machinji ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupitishwa na Baraza Kuu la Chadema, katika kikao chake kilichokaa jijini Mwanza.



Katika Kikao hicho cha Baraza Kuu kilichodumu hadi saa nne usiku Machi 12,2016 ambapo Freeman Mbowe alitangaza jina la Dk. Machinji na kuungwa mkono na wajumbe wa baraza hilo, hivyo anajaza nafasi iliyoachwa na Dk. Willibrod Slaa, aliyejienguwa ukatibu mkuu wa chama hicho.



Jina la Dk. Machinji halikuwa miongoni mwa wanachama wa Chadema ambao walikuwa wanatarajiwa kumrithi Dk. Slaa kwani waliokuwa wanatabiriwa kukalia kiti hicho ni Salum Ally Mwalimu, Frederick Sumaye, Benson Kigaila, John Mnyika, Dk. Marcus Albanie na Prof. Mwesiga Baregu.



Nafasi ya Katibu wa Chadema ilikuwa wazi tangu Dk. Slaa alipoondoka Chadema muda mfupi baada ya chama hicho kumpitisha Edward Lowassa aliyetokea CCM kuwa mgombea urais wa chama hicho na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527