MSAJILI WA HAZINA AZUNGUMZA NA MKURUGENZI MPYA WA HESLB




Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia (wa pili kushoto), katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Bill Kiwia (kushoto), akizungumza alipokuwa akitoa wasilisho lake kwa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu (kulia), katika kikao hicho.

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu (kushoto), akiagana na mgeni wake Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia (kulia), mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, katika kikao kilichofanyika Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM.

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kuzungumza na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Dkt. Bill Kiwia.

Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Msajili wa Hazina Aprili 25, 2024 Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujitambulisha kwa Menejimenti hiyo, kufuatia uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa HESLB.

Katika kikao hicho, viongozi hao wawili walijadiliana masuala mbalimbali yanayolenga kuongeza ufanisi na tija kwa kuzingatia falsafa ya R4 ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, katika kikao hicho Dkt. Kiwia aliwasilisha mikakati yake itakayowezesha taasisi hiyo kufikia malengo yake ya kuhakikisha vijana wengi wa kitanzania wanatimiza ndoto zao za kusoma elimu ya juu kwa kunufaika na mikopo wanayoitoa kwa manufaa ya jamii zao na Taifa kwa ujumla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post