FAHAMU FAIDA ZA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU NA MICHE BORA

Zikiwa zimebaki siku 5 kuelekea kusomwa kwa Bajeti ya Wizara ya Kilimo Bungeni kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 inayosubiriwa kwa shauku kubwa na wakulima nchini, tumekuandalia makala fupi uweze kufahamu faida za matumizi ya mbegu na miche bora katika kilimo cha kisasa na chenye tija.

1. Matumizi ya Mbegu na Miche bora husaidia mazao kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa kama vile joto kali au ukame.

2. Mbegu bora huzalisha matunda au mazao yenye virutubisho muhimu kwa afya za walaji na ladha nzuri.

3. Mbegu bora humsaidia mkulima  kupunguza gharama za matunzo kwasababu mimea inayotokana na mbegu bora huweza kujilinda dhidi ya magonjwa na wadudu.

4. Mbegu na Miche bora humuwezesha mkulima kupata mavuno mengi na yenye ubora unaokubalika katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Kutokana na faida hizo, Wizara ya Kilimo imeendelea kuhamisisha wakulima kutumia mbegu na miche inayozalishwa na Taasisi zinazotambulika nchini katika kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post