Na Mwandishi Wetu, Mikumi
Ujenzi wa Uwanja mpya wa Ndege wa kisasa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Morogoro umeendelea kukamilika ambapo leo kwa mara ya kwanza ndege zimeanza kupitia upande mmoja wa km 1 iliyokamilika kwa kuwekewa lami maalum (polymer).
Hayo yameshuhudiwa leo, Novemba 13, 2026, ambapo ndege zaidi ya 5 zilionekana katika hifadhi hiyo zikiwa zimeleta watalii waliokuja kujionea utajiri wa vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi huku majengo ya abiria, zima moto na mitambo mingine vikiwa vimekamilika tayari kupokea watalii wa AFCON 2027.
Uwanja huo mpya unajengwa miundombinu muhimu ikiwemo njia ya kuruka na kutua ndege (Runway) yenye urefu wa kilomita 1.8, ambapo kipande cha pili cha meta 800 kitakamilika kufikia Disemba 8, 2026, huku jengo la abiria kwa ajili ya huduma za kuingia na kutoka, eneo la zimamoto pamoja maeneo ya kupumzika na maegesho ya magari navyo vikiwa hatua za mwisho.












TAFUTA HABARI
Social Plugin