Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KISHAPU AELEZEA MAFANIKIO YA AFYA NA ELIMU



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Pili MnyemaMkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Niceforus Mgaya

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwasele 'B' Fabian Makongo

Na Sumai Salum-Kishapu


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amesema Serikali inaendelea kuweka nguvu katika kuboresha sekta za elimu na afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kupitia uwekezaji katika miundombinu, vifaa tiba na huduma za kijamii.


Mhe. Mhita ameyasema hayo Novemba 6, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, ambapo ameeleza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma muhimu za kijamii.


Akizungumzia sekta ya afya, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya, upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa pamoja na kuimarisha huduma za matibabu ili wananchi wapate huduma bora.


Amesema hatua hizo zinaenda sambamba na utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, ambao unalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu bila kukabiliwa na changamoto kubwa za gharama za matibabu.


Katika sekta ya elimu, ameeleza uwekezaji unaofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, akisisitiza umuhimu wa wananchi kuunga mkono jitihada hizo kwa kushiriki katika maendeleo ya elimu.

'Matokeo ya darasa la saba mwaka 2026 yameonesha dhahiri jinsi ambavyo uboreshaji wa miundombini katika sekta ya elimu kwa kushirikiana na msimamo wa wazazi na walezi wa Mkoa wetu wa Shinyanga ulivyofanikisha tukaingia tano bora huku shule mbili zikiwa ni za serikali na moja binafsi hakika nawapongezeni sana zaidi tuendelee kuwasaidia watoto wetu kwa kuwasimamia katika masuala ya elimu kwani wameonesha wana Shinyanga tunaweza' amesisitiza Mhita

Aidha, amegusia masuala ya miundombinu ya barabara, ikiwemo barabara ya Kolandoto, akieleza umuhimu wa kuendelea kuboresha miundombinu hiyo ili kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi kwa wananchi.











































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com