Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo mkoani Shinyanga imeweka rekodi nzuri katika Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) mwaka 2026, baada ya wanafunzi wake wote 109 waliofanya mtihani huo kufaulu kwa kupata Daraja A, sawa na asilimia 100 ya ufaulu.
Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), shule hiyo yenye namba ya usajili PS1704055 imepata wastani wa alama 279.7339 na kufanikiwa kupata Daraja A (Bora).
Katika matokeo hayo, wasichana 50 na wavulana 59 wamepata Daraja A, huku hakuna mwanafunzi aliyepata Daraja B, C, D au E.
Uchambuzi wa matokeo kwa kila somo unaonesha kuwa wanafunzi wa shule hiyo wamefanya vizuri katika masomo yote sita yaliyofanyiwa mtihani.
English Language imeongoza kwa wastani wa alama 48.8349 kati ya 50, ikifuatiwa na Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi iliyopata wastani wa alama 47.4128.
Masomo mengine ni Hisabati (47.3578), Sayansi na Teknolojia (45.9908), Uraia na Maadili (45.6514) na Kiswahili (44.4862).
Mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za pamoja za walimu, wanafunzi, wazazi na uongozi wa shule katika kuweka mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji.
Akizungumzia mafanikio hayo, uongozi wa shule umeeleza kuwa matokeo hayo ni faraja kubwa na chachu ya kuendelea kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa, huku ukitoa shukrani kwa walimu, wazazi na walezi kwa ushirikiano wao katika safari ya mafanikio ya wanafunzi.
Uongozi huo umeeleza kuwa shule itaendelea kuweka mkazo katika nidhamu, ubora wa ufundishaji, malezi bora na kukuza vipaji vya wanafunzi ili kuwaandaa kuwa viongozi na wataalamu wa baadaye.
Kwa mafanikio haya, Little Treasures Primary School inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kutoa elimu bora inayojenga maarifa, ujuzi na maadili kwa watoto.
Hongereni wanafunzi wote 109, walimu, wazazi na familia nzima ya Little Treasures Primary School kwa mafanikio haya!
Little Treasures Primary inafanya usajili wa darasa la kwanza kwa mwaka 2027 lakini pia kuna nafasi za masomo kwa darasa la Awali hadi darasa la 7 karibuni wote nafasi ni chache.
Namba za simu:
Mwl. Mkuu: 0623501979
Meneja: 0753122648
Mkurugenzi: 0767211531

TAFUTA HABARI
Social Plugin