
Wito huo unafuatia kauli za hivi karibuni za mwanamama huyo ambaye amekuwa akiwahimiza Watanzania kushiriki maandamano na vurugu nchini, huku akijitenga wazi na wazo la kuja kushiriki yeye mwenyewe.
Katika posti zake za mitandaoni, mwanamama huyo alifanya dhihirisho la wazi la kutokukabiliwa na matatizo yoyote , akijinadi kuwa hana sababu ya kuja kushiriki maandamano. Alijiuliza: "Mimi nateseka kitu gani na CCM mpaka nitoke Marekani nije mtaa? Nateseka namna gani?"
Alikiri waziwazi kufurahia maisha mazuri nchini Marekani, akitaja kuishi katika nyumba ya kifahari, kuendesha biashara inayomwingizia kipato, pamoja na kufurahia huduma za uhakika kama vile mfumo wa afya wa dharura wa 911 na kutokatika kwa umeme.
Kauli hizi zimezua maswali mazito kutoka kwa wachambuzi na Watanzania wa kawaida: Je, kweli mtu anayeishi katika "pepo" ya kisasa, iliyojengwa kwa miaka 300 kwa utulivu na kazi, ana nia njema na Watanzania anaowashauri kuharibu miundombinu na kuhatarisha maisha yao?
Wito wa Kutafakari na Kukataa Uchochezi
Wachambuzi wa masuala ya kijamii wanasema kauli za Mange Kimambi ni dhihirisho la wazi kwamba yeye anainjoi matunda ya nchi iliyotulia, yenye sheria, na iliyostawi, huku akiwataka wengine wateseke kwa ajili ya ajenda zake binafsi.
"Huyu ni kivuruge na mchochezi. Anawaza uharibifu huku yeye akifurahia usalama na amani ya Marekani," alisema mmoja wa wachambuzi. "Anatumia nafasi yake ya kuishi maisha mazuri kuwafanya Watanzania wa hali ya chini kuwa 'kete' katika mchezo wake wa kisiasa. Kila mtu anayeandika 'Njoo tuandamane!' akikwepa kuja yeye mwenyewe ni kinara asiye na shida wala ajenda ya dhati."
Watanzania wamehimizwa kufikiri kwanza na kuepuka kuwa daraja la kivuruge kufikia malengo yake ya kibinafsi.
Wito umekuwa ni kulinda amani ambayo haina bei, badala ya kuharibu miundombinu na mustakabali wa watoto kwa ajili ya maneno ya mtu anayeishi mbali na matatizo yao. Badala ya kubomoa, Watanzania wametakiwa kutumia nguvu na akili zao kujenga nchi yao, kwani nchi zilizostawi hazikujengwa kwa vurugu bali kwa kazi ngumu na utulivu.
"Tupinge kauli za uchochezi kwa kuthamini maisha yetu na Taifa letu kwanza. Haturuhusu mtu yeyote atumie nchi yetu kama uwanja wa michezo kwa masilahi yake binafsi," inahitimisha kauli hiyo.
Social Plugin