Sunday, January 1, 2017

LOWASSA,SUMAYE WAMTEMBELEA LEMA GEREZANI

Maziri  wakuu wa zamani ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, jana wamemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema katika Gereza Kuu la Kisongo mjini Arusha.

Lowassa akiongozana na Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye pia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika katika gereza hilo.

Calist alisema Lowassa alifika gerezani hapo saa tano asubuhi huku Sumaye aliyeongozana na Naibu Meya wa Arusha, Viola Lazaro akifika baadaye saa saba mchana.

Calist alisema Lowassa akizungumza na Lema, alimwambia kuwa mahakama ndiyo chombo pekee kinachoaminiwa na wananchi, hivyo kinapaswa kutenda haki kwa watu wote.

Alisema Lowassa aliridhishwa na afya ya Lema na kumtaka awe mvumilivu, hasa katika kipindi hiki anachokabiliwa na kesi na aliwataka wananchi wa Arusha Mjini kumwombea kiongozi huyo.

“Watanzania wana matumaini makubwa sana na mahakama, wanaamini chombo hiki pekee ndicho kitakachowapa haki yao, hivyo kwa mwaka 2017 mahakama itoe haki na kuendesha kesi bila upendeleo kwa sababu ndiyo sauti ya wanyonge, nakutakia amani na mwaka mpya mwema,” Calist alimnukuu Lowassa.

Kwa upande wake, Sumaye alisema kuwa alimtaka mbunge huyo kuwa jasiri katika kipindi hiki kwa sababu suala linalomkabili litafika mwisho.

“Mimi nilikuja tu kumsalimia, kumjulia hali ya afya yake kwa sababu Lema tangu amekaa huku gerezani nilikuwa sijapata nafasi ya kuja kumtembelea, kwa vile wakati huu niko katika maeneo haya ya Kaskazini, nikasema nije kumsalimia, afya yake nzuri na nimemuona hana wasiwasi, naona kabisa amekaa vizuri, ameelewa hiyo hali na amepokea, hana uso wa kusononeka na hilo limenipa moyo.

“Nimemwachia ujumbe ‘just be strong’ (awe jasiri), haya yote yatapita muda wake ukifika, suala lake liko mahakamani sio la kisiasa, hata kama lililomleta huku linahusiana na siasa, suala la dhamana tunatarajia litafika mwisho wake, lakini nimemwambia hata kama dhamana ikikosekana, bado kesi ya msingi itafika mwisho wake, asiwe na wasiwasi wala hamaki, awe jasiri asikate tamaa,” alisema.

Desemba 11, mwaka jana, Katibu wa Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, alimtembelea Lema katika gereza hilo na alimtia moyo aendelee na mapambano na kumtaka asikate tamaa ya kupigania haki za Watanzania.

Lema alikamatwa Novemba 2, mwaka jana akiwa nje ya Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na kufikishwa mahakamani Novemba 11, mwaka jana akikabiliwa na kesi za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli na hadi wakati huo bado anashikikiwa mahabusu katika gereza hilo.

Januari 4, mwaka huu Mahakama Kuu Kanda ya Arusha inatarajia kutoa uamuzi wa rufaa namba 135 ya mawakili wa Serikali waliyokata kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliompa Lema dhamana, hata hivyo uamuzi huo haukuweza kutekelezwa kwa sababu ya nia ya kukata rufaa waliyoitoa mawakili hao wa Serikali.

Tutumie Habari,Picha,Video,Tangazo,Ushauri n.k. Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0757478 553 ,0625 918 527

Malunde1 blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Share:

Tafuta Habari Hapa

Habari Kuu

Video: JINSI NAPE NNAUYE ALIVYOTISHIWA BASTOLA NA POLISI AKITAKA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI DAR

Mtazame hapo chini Mbunge Nape akiamriwa kurudi ndani ya gari mara tu alipofika katika Hoteli ya Protea kwa ajili ya kuzungumza na waandish...

Mshana Computer Solution

Mzee Dispensary- Shinyanga Mjini

Video: Mama Ushauri - Namhala

Bofya Hapa Kutazama Video

 Bofya Hapa

Habari 10 Zilizosomwa sana mwezi huu

Ungana Nasi Hapa

Maktaba Yetu ya Habari

Download Malunde1 blog App

 Bofya Hapa

Translate This Blog

Copyright © MALUNDE 1 BLOG | Powered by Malunde