BARRICK NORTH MARA RUNNERS CLUB YASHIRIKI KILIMANJARO MARATHON 2024

Barrick North Mara Runners Club, inayoundwa na wafanyakazi wa mgodi wa Barrick wa North Mara,ambayo imekuwa ikitamba katika mchezo wa mbio za marathon na kushiriki mbio mbalimbali,imeshiriki mbio za Kimataifa za Kilimanjaro 2024 zilizofanyika mkoani Kilimanjaro ambapo baadhi yao wamemudu kukimbia mbio za masafa marefu.

Kampuni ya Barrick inayo sera madhubuti katika kusaidia wafanyakazi kwenye upande wa michezo kwa kuwa na miundo mbinu ya mazoezi kama gym, swimming pool, uwanja wa mpira wa miguu , uwanja wa mpira wa kikapu pamoja na uwanja wa mpira wa pete. Pia inatoa vifaa na nyenzo mbalimbali za kufanyia mazoezi, vilevile kugharamia wafanyakazi kushiriki mashindano yanayofanyika nje ya migodi yake ikiwemo nje ya nchi.

Kampuni pia kupitia kitengo cha Afya na Usalama huwa inaandaa mashindano ya ndani kwa kushindanisha idara mbali mbali hii ni kama njia moja wapo ya kuweza kuweka vizuri afya za mwili na akili za wafanyakazi wawapo kazini.Kampuni imekuwa ikiandaa mashindano ya riadha yajulikanayo kama Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon.

Wafanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara uliopo mkoani Mara wakishiriki katika mashindano ya mbio za Kilimanjaro International Marathon yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro karibuni.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick North wakifurahia baada ya kushiriki mashindano ya mbio za Kilimanjaro International Marathon yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post