Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAWAKE JIVUNIENI KIPINDI HIKI CHA MAENDELEO MLICHONACHO KULIKO NYAKATI ZINGINE ZOZOTE - WAZIRI KAPINGA



📌Hii ni kutokana kazi kubwa anayoifanya Mhe Rais kuleta fursa za kiuchumi kwa wanawake;

📌Afungua kongamano la wanawake   Wa mkoa wa Iringa kwa mwaka 2026 lililowakutanisha wanawake zaidi ya 900;

📌Awaasa wanawake kuwa mabalozi wazuri kwenye mitandao ya kijamii kulinda utu na heshima;

📌 Ahimiza ukombozi wa wanawake kiuchumi na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.

IRINGA.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb), amesema katika kipindi ambacho wanawake wanapaswa kujivunia maendeleo yao ni  sasa kutokana na fursa nyingi za kiuchumi na kibiashara ambazo zinawalenga kwa kiasi kikubwa.

Waziri Kapinga ameyasema hayo mjini Iringa wakati akifungua kongamano la wanawake wa mkoa wa Iringa kwa mwaka 2026 lenye lengo la kuwakutanisha wanawake wote wa mkoa wa Iringa kujifunza na  kujadili fursa za kiuchumi na Wajibu wao Kama walezi kwenye Jamii.

Mhe Kapinga amesema Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fursa nyingi za kiuchumi kwa wanawake hasa katika kipindi hiki hivyo ni vema kujivunia kazi kubwa inayofanywa na yeye ikiwemo fursa za mitaji  ya kibiashara hususani kwa wajasiriamali wadogo na wa Kati  ambao wananufaika na fursa hizo 

Aidha Mhe Kapinga ameongeza kuwa ili kuunga mkono jitihada hizo Wizara ya Viwanda na Biashara ilizindua Sera ya maendeleo endelevu ya Viwanda na Sera ya maendeleo ya jasiriamali ndogo na za Kati sambamba na mkakati wake wa utekelezaji kwa lengo kuwainua wajasiriamali wadogo na wa Kati kiuchumi.

Katika hatua nyingine Mhe kapinga aliwataka wanawake kuwa mabalozi wazuri wa matumizi ya mitandao ya kijamii ili kulinda heshima utu na nidhamu na anatamani zaidi wanawake kujikita kwenye maendeleo ya kiuchumi zaidi kuliko kutumia mitandao hiyo bila tija.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa jukwaa hilo la wanawake kwa mwaka 2026 Dkt Tumaini  Msowoya amesema,wameamua kuwa na kongamano hilo ili kutoa fursa kwa wanawake kujifunza masuala ya kiuchumi, uwekezaji na kutoa elimu ya masuala mbalimbali .

Amesema zaidi ya wanawake 900 kutoka mkoa wa Iringa wamekutana kwenye kongamano hilo lililoandaliwa kwa pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa na kamati ya kongamano la wanawake mkoa wa Iringa kwa mwaka 2026

Miongoni mwa masuala waliyojinza  wanawake hao ni pamoja na masuala ya Afya ya akili na namna ya kukabiliana nayo, majukumu ya malezi kwa kina mama na fursa za uchumi na uwekezaji.


















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com