Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa kwanza kwa mara ya 10 mfululizo wa Tuzo za uandaaji bora wa vitabu vya hesabu zinazotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA) katika kundi la Taasisi za Wakala wa Serikali wanaotumia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta ya Umma (IPSASs).
Tuzo hizo zinatolewa leo Novemba 26, 2026 katika Hoteli ya APC Bunju Jijini Dar es Salaam ambapo kushinda kwa TRA kumetanjwa kutokana na umahiri wa Idara ya Fedha katika uandaaji wa vitabu vya hesabu.
Awali akizungumza katika hafla ya utoaji wa Tuzo hizo mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Mhe. Nsubili Joshua amezipongeza taasisi zilizoshinda na kutoa changamoto kwa taasisi nyingine kuwa mahiri katika eneo la kuandaa hesabu kwa viwango vya kimataifa.
TAFUTA HABARI
Social Plugin