Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JESHI LA MAGEREZA NA VETA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA URASIMISHAJI UJUZI KWA WAFUNGWA


Na Ssgt Mawazo Mtondo - DODOMA.

Mkuu wa Sehemu ya Viwanda wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Dkt. Uswege Mwakahesya, leo Novemba 18, 2026, ameongoza kikao cha maandalizi ya hafla ya kuwatunuku vyeti wafungwa 481 waliohitimu mafunzo ya ufundi kupitia Mfumo Usio Rasmi wa Mafunzo (RPL) chini ya Programu ya Mama Samia.

Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Novemba 2026 katika Viwanja vya Gereza Karanga, mkoani Kilimanjaro, na itahusisha pia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Ushirikiano huo unalenga kutambua, kuthibitisha na kurasimisha ujuzi wa wafungwa ili kuwawezesha kutumia ujuzi huo kujiajiri au kuajiriwa wanaporejea katika jamii.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com