Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : RC MBONI MHITA AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA BOAZ MARTINE SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Boaz Martine kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya familia eneo la Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga, nyuma yake ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Anorld Makombe - Picha na Kadama Malunde
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Boaz Martine kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya familia eneo la Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga
Boaz Martine enzi za uhai wake
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita akitoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Boaz Martine wakati wa ibada na shughuli za mazishi zilizofanyika katika Mtaa wa Kitangili, Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akitoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Boaz Martine wakati wa ibada na shughuli za mazishi zilizofanyika katika Mtaa wa Kitangili, Manispaa ya Shinyanga.
Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Boaz Martine kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya familia eneo la Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga.
Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Boaz Martine kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya familia eneo la Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga.
Waandishi wa habari pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Boaz Martine.
Shughuli za mazishi ya marehemu Boaz Martine zikiendelea katika makaburi ya familia eneo la Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga.
Shughuli za mazishi ya marehemu Boaz Martine zikiendelea katika makaburi ya familia eneo la Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga 
Shughuli za mazishi ya marehemu Boaz Martine zikiendelea katika makaburi ya familia eneo la Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita ameongoza mamia ya waombolezaji katika kuaga mwili na kushiriki mazishi ya mpiga picha na mwandishi wa habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Boaz Martine (25) aliyefariki dunia kufuatia ajali ya gari wakiwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mazishi hayo yamefanyika Alhamisi Mei 21, 2026 katika makaburi ya familia yaliyopo Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga, huku yakihudhuriwa na viongozi wa serikali, waandishi wa habari, ndugu, jamaa na wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.

Awali, ibada ya kumuombea marehemu imefanyika nyumbani kwa familia ya marehemu katika Mtaa wa Kitangili, Kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga na kuongozwa na Mashahidi wa Yehova.

Akizungumza wakati wa mazishi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imepoteza kijana mchapakazi aliyekuwa akitumia taaluma yake kuutangaza mkoa wa Shinyanga kupitia kazi zake za upigaji picha na habari.
“Tumempoteza kijana mwenye nidhamu, mchapa kazi na aliyekuwa akijituma kwa moyo mkubwa katika majukumu yake. Serikali ya Mkoa wa Shinyanga inaungana na familia, ndugu, jamaa pamoja na waandishi wa habari wote katika kipindi hiki kigumu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipe familia nguvu na faraja,” amesema Mhe. Mhita.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru amesema Boaz alikuwa kiunganishi muhimu kati ya waandishi wa habari na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali, akieleza kuwa upendo wake, ushirikiano na moyo wa kujituma vitaendelea kukumbukwa na wengi waliopata nafasi ya kufanya kazi naye.
Boaz Martine alifariki dunia Mei 19, 2026 kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Samuye mkoani Shinyanga, ajali iliyohusisha gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi alisema ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa dereva wa gari aina ya Toyota Harrier aliyekuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Katika ajali hiyo, watu saba walijeruhiwa ambao ni Frank Mshana Mwandishi wa ITV/Radio One, Johnson James, Koplo Swahiba Msangi, Neema Madono (36), Rehema Edson (45), Shadia Omari (32) pamoja na dereva wa gari la Land Cruiser Laurence Peter (34).

Majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga huku wengine wakitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita akitoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Boaz Martine wakati wa ibada na shughuli za mazishi zilizofanyika katika Mtaa wa Kitangili, Manispaa ya Shinyanga.

Shughuli za mazishi ya marehemu Boaz Martine zikiendelea katika makaburi ya familia eneo la Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com