MAGUFULI : WATANZANIA MNA RAIS KWELI KWELI,JIWE KWELI KWELI...SITISHWI NA SITISHIKI


Rais Dkt. Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea eneo ambalo watakula raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni.


Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa mkoa wa Singida muda mchache kabla ya kukizindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti Mount Meru Millers kilichojengwa mkoani humo.

"Nataka niwahakikishie watanzania kuwa mna Rais kweli kweli, jiwe kweli kweli. Sitishwi wala sitishiki mimi jukumu langu ni kwaajili ya watanzania, nikuhakikisha nawavusha watanzania kutoka mahali kwenye shida na kwenda mahali kwenye raha. 

Ninajua hiyo ndio itakuwa sadaka yangu kwa watanzania ili kusudi hata siku moja nikienda huko mbinguni Mungu atakaponihitaji, akanichague kutokana na mimi nilikuwa kiongozi mzuri hivyo unaweza hata kuongoza Malaika polepole kwasababu ninajua kuna maisha baada ya maisha ya hapa duniani", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "ndio maana nawaomba sana viongozi wa dini, masheikh na wale watu mbalimbali katika imani zao tuitangulize Tanzania kwanza, tusitumike".

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Magufuli amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikomboa na kujiongezea kipato cha maisha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527