WASANII WAGUSWA HUKUMU YA SUGU..WADAI SIYO PICHA NZURI KWA NCHI


Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na mwenzake Emmanuel Masonga wamehukumiwa kwenda jela miezi mitano na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya leo Februari 26, 2018 baada ya kukutwa na hatia kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli.

Baada ya kuhukumiwa kwenda jela baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva wamefunguka yao ya moyoni kuhusu tukio hilo huku wengine wakimtia moyo kuwa gerezani siyo kaburini hivyo atamaliza muda wake na kurudi uraiani kuwapigania wananchi wa Mbeya.

"Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini 'stay strong' Jongwe" aliandika Niki wa Pili 

Kwa upande wake msanii Rama Dee yeye amesema kuwa ameumizwa sana na bahari ya Sugu kufungwa jela miezi mitano na kudai si picha nzuri katika nchi yetu kwa mambo kama haya. 

"Nasikitika sana kwa hii habari kama msanii pia kama rafiki wa Sugu, hii si picha nzuri" Rama Dee 

Aidha msanii Izzo Bizness ambaye anaiwakilisha Mbeya vizuri katika muziki wa Hip hop pia ameonyesha hisia zake na kumtaka Mbunge huyo kuwa mvumilivu na kusimama imara katika kipindi hiki.

Mbali na huyo Rapa Roma Mkatoliki alikuwa na haya ya kusema juu ya kifungo cha Sugu "Hata hili litapita' stay strong Joseph Zaburi 35: 1-28 "

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527