JINSI RAIS MAGUFULI ALIVYOENDESHA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA CHATO

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli jana alisali Ibada ya Jumapili ya 15 ya mwaka wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita na kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.


Katika harambee hiyo Mhe. Rais Magufuli ambaye aliongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli alifanikiwa kuchangisha fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 13, ahadi Shilingi 920,000/=, mifuko ya saruji 33 na malori 2 ya mchanga.


Mhe. Rais Magufuli aliwapongeza waumini wa Parokia ya Chato kwa hatua kubwa waliyopiga katika ujenzi wa kanisa kuu la Parokia hiyo na amewataka kuendelea kujitolea kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi huo.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.