WANAFUNZI WA CHUO CHA UALIMU SHYCOM NA CHUO CHA UUGUZI KOLANDOTO SHINYANGA WACHEZA MICHEZO YA KIRAFIKI


Wachezaji timu ya wanawake Kolandoto wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga-Picha zote
na Philipo Chimi-Shinyanga

Wachezaji timu ya wanawake Shycom

Timu ya Kolandoto kushoto,Shycom kulia
 Walimu kutoka Kolandoto wakiwa uwanjani
Mchezo wa netball unaendelea
 Shycom wakishangalia
Mpira wa miguu unaendelea
Mchezo unaendelea
Mpira wa kikapu unaendelea
Chuo cha ualimu mkoani Shinyanga  SHY COM jana kiliibuka kidedea katika michezo ya kirafiki dhidi ya timu kutoka Chuo cha uuguzi Kolandoto mkoani Shinyanga michezo iliyopigwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.

Katika michezo hiyo ya kirafiki mchezo wa kwanza ulikuwa ni mpira wa pete (netball)ambapo timu ya chuo cha ualimu Shinyanga ilitoa dozi ya kuchapa bao 18 kwa sifuri timu ya netball kutoka Chuo cha uuguzi Kolandoto.

Katika mchezo huo mchezaji machachari wa timu ya netball Shycom Ratifa Hussein  ndiye alikuwa wa kwanza kufungua pazia hilo la mvua ya magoli kwa tim yake baada ya kufunga goli safi na hivyo kuonekana kuwa tishio kwa mabeki wa timu ya netball ya kutoka Kolandoto.

Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi kinapulizwa timu ya Shycom magoli 18 Kolandoto 0.

Baada ya mchezo huo kuisha ulifuatiwa mchezo wa wavu (Volleyball) ambao ulichezwa dakika zote zikamalizika kwa sare ya timu hizo kufungana seti moja kwa moja.

Kufuatia hali hiyo ilimlazimu mwamuzi kuongeza muda ili mshindi kupatikana na hatimae tim ya moira wa wavu kutoka chuo cha uness kolandoto kuibuka na ushindi wa seti mbili kwa moja.

Mchezo uliofuatia ulikuwa ni mpira wa kikapu ambapo shycom walikubali kupokea kichapo cha kufungwa vikapu 28 kwa 8 na hivyo kufanya Kolandoto kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

 baada ya mchezo huo ulifuatiwa mchezo wa watu wazima mpira wa miguu ambapo shycom walifanikiwa kuichapa kolandoto kipigo cha mbwa mwizi kwa kuifunga goli 4 kwa nunge .

Magoli ya Shycom yaliwekwa kimyani na Ramadhani Songolo dakika ya 10 kipindi cha kwanza ,goli la pili lilifungwa na Kasungu Kashindye dakika ya 15 kabla ya Bandoma Mtata kuongeza bao la tatu dakika ya 40 kipindi cha kwanza.

 Baada ya mapumziko Ramadhani Songolo kwa mara nyingine akaongeza msumari wa nne na kuifanya Shycom kuongoza goli 4 kwa 0 ,hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Shycom 4 Kolandoto 0. 

Baada ya mchezo kumalizika makaptain wa timu zote mbili  Valentina Malima kutoka Shycom na Jacob  Phaustine kutoka Kolandoto walisema mchezo ulikuwa mzuri aliyepoteza kapoteza kwani  mchezo  ndivyo ulivyo.
Na Philipo Chimi-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527