Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAMASHA LA VIJANA ‘TWEN’ZETU KWA YESU 2025’ KUWASHA MOTO WA INJILI CCM KAMBARAGE - SHINYANGA

Mratibu ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Odolous Gyunda akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Julai 25, 2025 - Picha na Kadama Malunde
Mratibu ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Odolous Gyunda akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Julai 25, 2025

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (DKMZV) , linalojumuisha mikoa ya Shinyanga na Simiyu, kwa kushirikiana na Kituo cha Matangazo Jambo FM, limeandaa Tamasha la Vijana la Twen’zetu kwa Yesu 2025 – Msimu wa Pili, litakalofanyika Agosti 16, 2025 katika Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

Tamasha hilo linalobeba kauli mbiu ya "Ishi kwa Malengo" linatarajiwa kuwa jukwaa maalum la uimbaji wa nyimbo za Injili, likiwa na lengo la kuwajenga vijana kiimani, kiakili na kijamii kupitia ujumbe wa nyimbo, maombi, mafundisho ya Neno la Mungu, burudani safi ya kiroho na ushirika wa pamoja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Julai 25, 2025, Mratibu ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Odolous Gyunda, amesema mgeni rasmi katika tamasha hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Mboni Mhita, huku Mnenaji Mkuu akiwa ni Mhashamu Askofu Jackson Sosthenes wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam.

“Tamasha hili ni mahsusi kwa vijana, lakini kila mtu anakaribishwa. Hii ni siku ya ibada, burudani ya kiroho na utukufu kwa Mungu. Hatutakuwa na siasa, ni tukio la kutamtangaza Yesu Kristo na kumwimbia Mungu” ,amesema Mchungaji Gyunda.
Mratibu ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Odolous Gyunda

Kwa mujibu wa Mchungaji huyo, tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa waimbaji na vikundi mbalimbali maarufu na vya kusisimua kutoka ndani na nje ya mikoa ya Shinyanga Simiyu.

Baadhi ya watakaotumbuiza ni AGAPE Gospel Band kutoka Dar es Salaam, Neema Gospel Choir ya Dar es Salaam, Boaz Danken kutoka Mwanza, AICT Kambarage Choir ya Shinyanga, na Malaika Wakuu kutoka Kanisa Katoliki Ngokolo, Shinyanga.

Aidha, kutakuwepo na kwaya za vijana kutoka KKKT – DKMZV, Kwaya ya Sungusungu,pamoja na mbio za baiskeli ambazo zitachangamsha tamasha hilo.

“Kupitia tamasha hili tutawainua pia waimbaji chipukizi. Ni fursa ya kipekee kwa vijana kutangaza vipaji vyao huku wakimtumikia Mungu,” ameongeza Mchungaji Gyunda.

Katika kuakisi hali ya taifa, amesema siku hiyo itatumiwa pia kwa ajili ya maombi maalum ya kuombea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Happiness Yoram , amesema tamasha hilo limebeba malengo makubwa ya kuwaunganisha vijana na jamii kwa ujumla kupitia nyimbo za Injili na maombi ya pamoja.
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Happiness Yoram. 

“Hili ni jukwaa la kiroho kwa vijana, lakini pia kwa watu wote wanaotamani kushiriki ibada ya nguvu. Tunawaalika kwa moyo wote wakazi wa Shinyanga na mikoa jirani kama Simiyu, Geita na Mwanza kujitokeza kwa wingi,” amesema Bi. Happiness.

Aidha, ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa sekta binafsi, taasisi za kidini na mashirika ya kijamii kujitokeza kudhamini tamasha hilo, ili kusaidia ujumbe wa Neno la Mungu kuwafikia watu wengi zaidi kwa mafanikio makubwa.

Ameeleza kuwa maandalizi yote yanakwenda vizuri na tayari tiketi za kuingia zinapatikana kwa shilingi 5,000, huku tisheti rasmi za tamasha zikauzwa kwa shilingi 20,000 akibainisha kuwa tiketi na tisheti zinapatikana katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Shinyanga, Kahama na Bariadi mkoani Simiyu.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Vipindi wa Jambo Media, Bw. Renatus Kiluvia, amesema kuwa Jambo Media inajivunia kuwa mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo, akieleza kuwa litakuwa tukio la kipekee litakalobeba uzito wa kiroho kwa wakazi wa mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
Msimamizi wa Vipindi Jambo Media, Renatus Kiluvia.

“Tamasha hili si la kawaida. Tunatarajia kuwa sehemu ya historia ya kiroho itakayogusa maisha ya watu, hasa vijana. Jambo Media ipo bega kwa bega kuhakikisha ujumbe wa Injili unafika mbali kupitia tamasha hili,
” amesema Kiluvia.

“Tamasha la ‘Twen’zetu kwa Yesu 2025’ ni zaidi ya burudani. Ni sehemu ya maisha, maombi na kusanyiko la matumaini kwa vijana wetu na jamii kwa ujumla,” ameongeza Kiluvia.
Mratibu ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Odolous Gyunda akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Kadama Malunde
Mratibu ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Odolous Gyunda akizungumza na waandishi wa habari 
Mratibu ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Mchungaji Odolous Gyunda akizungumza na waandishi wa habari 
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Happiness Yoram akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Julai 25, 2025
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Happiness Yoram akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Julai 25, 2025
Chaplin wa KKKT Kanisa Kuu la Ebenezer Shinyanga ambaye ni Mratibu wa Tamasha Twen’zetu kwa Yesu 2025, Mchungaji Nzinyangwa Mkiramweni akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Julai 25, 2025
Chaplin wa KKKT Kanisa Kuu la Ebenezer Shinyanga ambaye ni Mratibu wa Tamasha Twen’zetu kwa Yesu 2025, Mchungaji Nzinyangwa Mkiramweni akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Julai 25, 2025
Chaplin wa KKKT Kanisa Kuu la Ebenezer Shinyanga ambaye ni Mratibu wa Tamasha Twen’zetu kwa Yesu 2025, Mchungaji Nzinyangwa Mkiramweni akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Julai 25, 2025
Msimamizi wa Vipindi Jambo Media, Renatus Kiluvia akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Julai 25, 2025
Msimamizi wa Vipindi Jambo Media, Renatus Kiluvia akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, Julai 25, 2025




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com