Wapenzi wa muziki wa asili na uhalisia wamepata zawadi murua kutoka kwa wakali wa sauti na tungo, Mayiku Sayi kwa kushirikiana na Limbu Luchagula, kupitia wimbo wao mpya uitwao “Jiwe La Gizani”, ambao tayari umeachiwa rasmi kwa video ya kiwango cha juu cha 4K kupitia Migera Studio.Wimbo huo unatajwa kuwa ni miongoni mwa kazi bora zilizobeba maudhui ya maisha halisi, changamoto, mafumbo yenye hekima, pamoja na ujumbe wa kijamii unaobeba hisia za mamilioni ya watu. “Jiwe La Gizani” ni kazi inayochanganya utunzi mzito, mdundo wa kuvutia na uchezaji wa video uliopangiliwa kitaalamu, na tayari mashabiki mitandaoni wameanza kuisambaza kwa kasi.
Mayiku Sayi, anayejulikana kwa uandishi wake wa kina na sauti yenye mvuto wa kipekee, ameendelea kuonesha ubora wake kwa kushirikiana na Limbu Luchangula – msanii mwenye mbinu kali za kisanaa na uwasilishaji wa sauti ya kipekee.
Wawili hao wametengeneza wimbo unaobeba tafsiri ya methali maarufu ya Kiswahili: “Jiwe haliendi gizani bure.”
Video ya wimbo huu imeandaliwa na Migera Studio, ikionesha mandhari ya kiasili, ubunifu wa hali ya juu, na maelezo ya picha yanayoongeza thamani ya ujumbe wa wimbo.
Social Plugin