Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATUHUMIWA 125 WAKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI MKOANI SHINYANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakamata watu 125 wanaotuhumiwa kuhusika na makosa mbalimbali katika kipindi cha kuanzia mwezi Juni hadi Julai 22, 2025.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 23, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amesema operesheni hizo zimehusisha ukamataji wa watuhumiwa wa makosa ya kutumia na kusambaza dawa za kulevya pamoja na wizi wa mali mbalimbali.

Katika operesheni hizo, dawa za kulevya zilizokamatwa ni pamoja na bhangi gramu 2,261, mirungi kilo 29, pamoja na pombe ya moshi lita 142.

Aidha, vitu vingine vilivyokamatwa ni pikipiki 22, mabati 16, nondo vipande 17, vitanda 4, redio 08, runinga 07 na bajaji 01 ambazo ni mali za wizi na nyingine hazina usajili.

Kamanda Magomi amesema kuwa operesheni hizo zinaendelea kwa lengo la kuhakikisha jamii inakuwa salama dhidi ya vitendo vya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na vitendo viovu vinavyofanyika katika maeneo yao.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com