Saturday, November 22, 2014

Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA 9

  Unknown       Saturday, November 22, 2014

Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya TISA  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi


SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 9

 MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
 timotheomathias0@gmail.com

Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi

-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE‬ ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa

Ilipoishia.......................

Vijana wengine watano waliletwa katikati tukawa vijana sita, na mbele yetu vikakeletwa nyungo sita. Mchawi mmoja alikuja akiwa amebeba visigino vya binadamu na kuanza kutugawia kila mmoja wetu alienea.
Kisigino kilikuwa kibichi kilionekana kimetoka kukatwa muda si mrefu kutoka kwa binadamu.

Mkuu wa wachawi alianza kutuelekeza na kutupa masharti alisema, kisigino ndiyo rimoti yenu, pia na matumizi yake alituelekeza.

Alitusisitiza kuwa tusipite karibu na kanisa la aina yoyote.
Kila mmoja wetu alikaa kwenye ungo wake tayari kwa safari ya kwenda Nigeria.....
Endelea ...........

Tukiwa tumekaa tayari kwa ajiri ya safari, bibi aliyetugawia nyungo alikuja kwa haraka sana akiwa anahema sana na kuanza kusema:

 "Wasiondoke kwanza maana hawajafanya tambiko la mwisho"
Katika sehemu tuliyokuwa tumekaa watu wote walikaa kimya ili kumsikiliza bibi anachozungumza. 
Mchawi mmoja wa kizungu alichomoka kutoka katikati, mkononi akiwa ameshikilia panga kali sana, alienda moja kwa moja mpaka sehemu alikokuwa amesimama yule bibi.
Bibi alikuwa na nywele ndefu sana kichwani,mzungu alipofika kwa bibi alishika nywele za bibi na panga lake lilitua shingoni mwa bibi na kukitenganisha kiwiliwili na kichwa.

Maeneo tuliyokuwa tumekaa yalitapakaa damu ya bibi aliyekatwa panga na mchawi mzungu.
Mpenzi msomaji wa stori hii, kwa macho yangu sikuweza kuamini nilichokiona machoni mwangu, baada bibi huyo kutenganishwa kiwiliwili na kichwa nilishangaa kuona kiwiliwili kubaki kimesimama takribani dakika mbili na pia kiliweza kutembea hatua tatu baadaye kilianguka na kuanza kudundadunda takribani dakika 6 baadae kilitulia tuli.
Upande wa kichwa alibaki nacho mzungu na kuanza kunywa damu.

Damu ilipoganda kichwa alikitupa chini karibu na kiwiliwili, visigino na mikono ya bibi vilikatwa na bibi alibebwa na kwenda kupikwa kwa ajili ya msosi.
Mzungu alipomaliza aligeukia upande wetu na watu wote walipiga makofi ishara ya kumshuru lakini mimi nilivyokuwa kauzu sikupiga makofi nilibaki namtumbulia mimacho tu.

 Mdomo wake ulitapakaa damu mpaka nguo aliyokuwa amevaa.
Kumbe kipindi sikumpigia makofi aliniona, alichokifanya alikuja moja kwa moja sehemu niliyokuwa nimekaa.
 Aliponisogelea nilihisi kama shoti ya umeme imetokea mwilini mwangu ,maana nilirushwa juu kwa kasi ya ajabu nikarudi chini na kufikia kichwa na kusimama harakaharaka na kuanza kupiga makofi kama chizi.

*****************
Baada ya hapo tulikwenda njia panda kuu ya Tanzania kwa ajili ya tambiko la mwisho, nikiwa kwenye usafiri wangu binafsi (ungo) na rimoti ya kisigino chako cha mguu nilitua taratibu njia panda na kujumuika na wengine.

Wakati  tunafanya tambiko pale njia panda, basi la aina yoyote lenye abiria lazima sehemu hiyo likifika lipate ajali na damu za abiria tunatumia wakati huo huo.

Kama gari la abiria halitatokea kwa wakati basi ujue kuna watu spesho kwa ajili ya damu.
Tukiwa katikati ya njia panda watu sita tulioteuliwa kwenda Nigeria tuliwekwa kati na kuambiwa tukae ikiwa wao wamesimama.

Mmoja wao alikuja na kuanza kutugawia mabakuli yaliyojaa damu za watu.
Baada ya hapo tukaletewa nyama za binadamu mbichi nikiwa zinatoa damu.

Hakuna ubishi tulikula na kunywa damu mpaka tukamaliza.
Tulipomaliza kula na kunywa tuliambiwa na kuahidiwa kuwa atakayekuwa wa kwanza kufika atapewa zawadi.

Unaambiwa kutoka Tanzania mpaka Nigeria unatakiwa ufike ndani ya dakika 6, maana nyungo zimesetiwa hivyo, ukizidisha dakika 6 wewe itakuwa halali ya wananchi kutoka duniani.
Kipindi hicho mkojo ulikuwa umenibana sana ilinibidi nichomoke kimya kimya kwa kitendo cha haraka nilijificha nyuma ya msitu na kuanza kukojoa. 

Nihisi kama kuna kitu kwa nyuma kinanigusa taratibu shingo niligeuka nilishtuka baada ya kumuona babu aliyegeuzwa kuwa kuku na mkuu wa wachawi yupo nyuma yangu,Duh nilitoa macho kama chura kabanwa mlango....
Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post