MAZISHI YA MANJU JAMES MAKUNGU SOMBI YATIKISA, NI MSIBA USIO NA VILIO! MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA...NI MAAJABU

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu James Makungu Sombi
Picha iliyotumika kuaga mwili wa James Makungu Sombi

TAZAMA VIDEO AKIAGWA KIMILA...NI MAAJABU
Mwili wa marehemu James Makungu Sombi
Mwili wa James Makungu Sombi ukiagwa kwa ngoma za kimila

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Ni msiba usio na vilio!!, Kuaga kwa picha tu bila kuona mwili wa marehemu!! Ndivyo mwili wa aliyekuwa Manju maarufu James Makungu Sombi (89) ulivyoagwa na kuzikwa huku ngoma za utamaduni wa Kabila la Wasukuma (Bhugobogobo na Bhununguli) zikichezwa ikiwa ni kutimiza agizo la manju huyo,ambaye ni mtaalamu wa masuala ya utamaduni na miongoni mwa waanzilishi wa makumbusho ya utamaduni wa Wasukuma Bujora mkoani Mwanza.

Mazishi ya James Sombi yamefanyika leo jioni Jumamosi Machi 3,2023 katika kitongoji cha Shikoba kijiji cha Mwamanga kata ya Mwamanga wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Awali mwili wa marehemu JameS Makungu Sombi uliagwa katika Makumbusho ya Bujora Ijumaa na leo Jumamosi kuagwa na mamia ya waombolezaji nyumbani kwake Kissa Mwanza ikiwa ni siku tano zimepita tangu afariki dunia Februari 27,2023 mchana baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake akisumbuliwa na Presha.

Enzi za uhai wake, James Sombi maarufu Ng’wana Sombi aliagiza kuwa akifariki dunia asizikwe hadi siku tano zipite na wakati wa kuaga mwili wake na wakati wa mazishi ngoma za utamaduni zichezwe na asiyepo mtu yeyote wa kulia bali zinazopaswa kulia ni ngoma pekee lakini pia hakutaka waombolezaji waage mwili wake kwa kuangalia mwili bali picha tu, na ameagwa kwa picha tu.

James Makungu Sombi aliyezaliwa tarehe 05.02. 1934 Mwamanga Magu ambapo alisoma shule ya msingi Kitongo kisha kuanza kujishughulisha na kilimo na ufugaji huko Shikoba- Mwamanga Simu Magu (zamani Kwimba) na baadaye alihamia Kisesa Mwanza akifanya kazi MWATEX baadaye kwenye makumbusho ya Bujora baada ya kufahamiana na Padre Clement waliyefahamiana tangu mwaka 1954 akawa anatangaza utamaduni wa Kabila la Wasukuma hadi Ulaya hasa Denmark na mwaka 2005 alistaafu kazi hapo kwenye Makumbusho ya Bujora.

James Sombi ameacha mjane, watoto 31, wajukuu 81 na vitukuu 72.

TAZAMA KILA KITU HAPA
Mwili wa marehemu James Makungu Sombi ukiwa nyumbani kwake Kisesa Mwanza
Mwili wa marehemu James Makungu Sombi ukiwa nyumbani kwake Kisesa Mwanza
Historia fupi ya marehemu James Makungu Sombi ikisomwa
Ngoma ya kimila Bhugobogo ikichezwa kwenye msiba wa  James Makungu Sombi 

Ngoma ya kimila Bhugobogo ikichezwa kwenye msiba wa  James Makungu Sombi 
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye ni mdau wa masuala ya utamaduni kupitia mtandao wa Malunde 1 blog akitoa pole na salamu za rambirambi kwenye msiba wa  James Makungu Sombi 

Kiongozi w dini akitoa neno kwenye msiba wa  James Makungu Sombi 
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu James Makungu Sombi  likiwa na picha ya kimila, kitambaa cheusi na chekundu wakati wa kuaga 
Msaidizi wa Mtemi wa Bhuhungukila, Fumbuka Samson Lubasa ambaye ni mwalimu wa utamaduni katika chuo cha Butimba TTC na mwanakamati wa Bujora Research Committee akiongoza zoezi la kuaga kimila mwili wa marehemu James Makungu Sombi 

 Zoezi la kuaga mwili wa marehemu James Makungu Sombi likiendelea

Zoezi la kuaga mwili wa marehemu James Makungu Sombi likiendelea kwa ngoma za kimila

Zoezi la kuaga mwili wa marehemu James Makungu Sombi likiendelea
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu James Makungu Sombi likiendelea
Wajukuu wa marehemu James Makungu Sombi wakiwa wamebeba jeneza la babu yao
Wajukuu wa marehemu James Makungu Sombi wakiwa wamebeba jeneza la babu yao
Wacheza ngoma ya Bhununguli wakipanda gari  liliobeba mwili wa marehemu James Makungu Sombi 
Mwili wa marehemu James Makungu Sombi ukiwa ndani ya gari baada ya kuwasili kijijini kwao Mwamanga Magu kwa ajili ya mazishi
Ngoma ya kimila ikiendelea wakati wa mazishi ya marehemu James Makungu Sombi  katika kijiji cha Mwamanga Magu 

Mwili wa marehemu James Makungu Sombi  ukiagwa katika kijiji cha Mwamanga Magu 

Waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa James Makungu Sombi

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments