Video : MANJU INAGA MLYAMBELELE NA NGELELA WATUNISHIANA MISULI... HAWA WASUKUMA BALAA

Kumekuwepo mpambano wa aina yake kati ya Ma Manju maarufu wa Kabila la Kisukuma kutoka mkoani Shinyanga Inaga Mlyambelele "Ntemi wasi"  na Manju Ngelela 'Ng'winikili Magulya' kupitia nyimbo zao walizozitoa hivi karibuni walizozipa jina la Katoro.

 Alianza Ngelela kwa kumnanga Inaga jinsi alivyomshinda kwenye moja ya mapambano yao ya ngoma Katoro mkoani Geita. Ngelela alionesha majigambo ya hali ya juu jinsi alivyomcharaza Inaga kwenye pambano lao huko Katoro... Sasa Desemba 29,2019 Inaga Mlyambelele kaachia Ngoma ya Mashambulizi dhidi ya Ngelela.

 Inaga amejinasibu jinsi alivyo mbabe na gwiji akijibu mapigo ya Ngelela. Nimekuwekea Ngoma ya Ngelela jinsi alivyohenyesha Inaga,kisha utazame Ngoma ya Inaga alivyojibu mapigo anasema kamtumia tu salamu,ajiandae show kamili mwaka 2020..

Pata burudani hapa chini wewe mpenzi na mdau wa ngoma za asili..Pata Uhondo wote kwa Magwiji hawa nyimbo za Kisukuma.
Video : Ngelela - Katoro

Video : Inaga Mlyambelele - Katoro

Video : Inaga Mlyambelele - Ngelela Ng'wanawane

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527