OJADACT YALAANI MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI

Picha ya Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28) mkazi wa Kirumba jijini Mwanza usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022 kisha naye kujiua

TAMKO LA KULAANI MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI, 31, MEI, 2022 

Chama  Cha  Waandishi wa  Habari  wa Kupiga  Vita  Matumizi  ya  Dawa  za Kulevya  na Uhalifu  Tanzania (OJADACT) kimefuatilia  kwa karibu  matukio ya  mauaji  yanayoendelea   hapa  nchini  na  kinachukua  nafasi hii  kulaani  matukio  hayo  ya  mauaji   kwa kuitaka  jamii  kutojihusisha  nayo.
Matukio  hayo  yamegawanyika  katika  makundi   mbalimbali ,  yapo  mauaji   yaliyofanyika kwa  sababu  za kimapenzi, tuhuma za wizi   na imani za kishirikina.

Visa  mkasa hivyo  vyote  vimesababisha  baadhi  ya watanzania  wenzetu  kutolewa  uhai wao  kinyume  na  sheria  za  nchi, ikiwemo  Katiba ya  Jamhuri  ya  Muungano wa Tanzania  ibara 14 inayotoa  haki ya  mtu  kuishi.

OJADACT inatoa mapendekezo  yafuatayo  kwa watanzania, Serikali na  Taasisi  mbalimbali.
Serikali ifanye  tafiti za kina  za kubaini chanzo  za mauaji  yanayoendelea nchini  pamoja  na kuwa na mpango wa kuanzisha  vituo  vya kisaikolojia.

Wanandoa watarajiwa  wawe na  muda  wa kujuana  tabia kwa undani  kabla ya  kuoana  na kufuata mifumo   rasmi  ya  usuluhishi wa matatizo yao

Jeshi  la  Polisi  litoe elimu sahihi  ya  matumizi  ya  silaha  kwa wamiliki wa silaha  nchini. 
Wazazi  wahakikishe wanajihusisha  na malezi ya watoto wao na  kuepuka kuwaacha  watoto  wajilee  kimaadili.
 
 Edwin    Soko 
 Mwenyekiti .
 OJADACT


 
Soma pia :


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post