MKURUGENZI WA CECY TOTO SHOP ATAKA WAZAZI KUSHIRIKIANA KATIKA MALEZI


Mkurugenzi wa Cecy Toto Shop, Cecilia Aikael amewataka wazazi kuambatana pamoja katika kufanya manunuzi ya bidhaa za watoto na hata kwenda Kliniki pamoja.

Cecy amesema wazazi wanapo ambatana pamoja inamsaidia mama kuwa mtulivu na huondoa msongo wa mawazo usiokuwa na sababu za msingi.

Amesema katika upande wa malezi na makuzi wazazi wanatakiwa kuwanunulia vifaa vinavyomsaidia mtoto kuchangamka ambavyo vinaendana na umri wa mtoto.

"Katika ukuaji wa mtoto kuna hatua unahitaji kuanza kujua kama mtoto anauwezo wa kusikia,hapo unampa kifaa kinachotoa mlio na pia unatakiwa kumuwekea rangi tofauti tofauti tofauti ili kujua anavutiwa na rangi zipi", amesema Cecy.

Cecy Toto Shop ni miongoni mwa wadhamini wa Usiku wa Waandishi na Wadau Wa Habari unaotarajiwa kufanyika tarehe 03/06/2022

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post