AKAMATWA TUHUMA ZA KUMPA KICHAPO MKEWE KISHA KUMWINGIZIA PANGA SEHEMU ZA SIRI ISHU YA MICHEPUKO

 

Picha haihusiani na habari hapa chini
**

Wakati mwingine unaweza usiamini lakini ndivyo ilivyotokea,Gabusi Mrimi (42)mkazi wa kijiji cha Nyahende Wilaya ya Serengeti anashikiliwa kwa tuhuma za kumpiga mke wake jina limefadhiwa kisha kumwekea panga sehemu za siri chanzo ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Longinus Tibishubwamu akiongea kwa njia ya Simu na Serengeti Media Centre akielekea Mwanza alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mei 25 majira ya saa 12 jioni mwaka huu nyumbani kwa mtuhumiwa akimtuhumu mke wake kuchepuka nje ya ndoa.


Amesema mtuhumiwa huyo ambaye kwa muda mrefu alikuwa Katoro Geita kwenye shughuli zake,aliporejea alimtuhumu mke wake kuwa si mwaminifu na kumfungia ndani kisha akaanza mshambulia kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili kisha akamwingizia panga sehemu za siri ili akiri.


Kamanda alikiri mtuhumiwa kukamatwa kwa ushirikiano na wananchi na Jarada Tayari liko kwa mwanasheria kwa upelelezi na majeruhi alikimbizwa hospitali ya Nyerere kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.


Chanzo - Serengeti_media_centre

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments