
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kahama cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Picha na Kadama Malunde
Meya wa Manispaa ya Kahama, Mataruma Kaniki Maganyala, akizungumza wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kahama cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Mbunge wa Jimbo la Kahama, Benjamini Ngayiwa, akizungumza wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kahama cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Frank Nkinda akizungumza wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kahama cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Na Kadama Malunde, Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ameipongeza Manispaa ya Kahama kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo, akisema mafanikio hayo yanaonesha uimara wa usimamizi wa fedha za umma na mshikamano wa viongozi wa halmashauri.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Mhita alisema Manispaa ya Kahama imeonyesha mfano mzuri wa uwajibikaji.
"Kwa miaka mitatu mfululizo mmepata hati safi. Ninawapongeza sana kwa namna ambavyo mmeendelea kubuni vyanzo vya mapato. Hakikisheni mapato hayo yanatumika vizuri na ongezeni kasi ya kujibu hoja zilizobaki ili zifungwe," amesema.
Amesema umoja na ushirikiano uliopo miongoni mwa viongozi wa manispaa hiyo umechangia mafanikio hayo, huku akipongeza ongezeko la mapato ya ndani kutoka shilingi bilioni 9 hadi bilioni 12.
Mhita pia amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu suala la ujenzi wa barabara za Kahama na kwamba wananchi wataanza kuona matokeo ya jitihada hizo katika kipindi kifupi kijacho.
Mbunge wa Jimbo la Kahama, Benjamin Ngayiwa, ameipongeza Manispaa ya Kahama kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa CAG, akisema mafanikio hayo ni kielelezo cha uwajibikaji, ushirikiano na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma.
Amesema hati hiyo imeongeza imani kwa wananchi na kuwataka viongozi pamoja na watendaji kuendelea kulinda mafanikio hayo kwa kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuleta matokeo chanya kwa wananchi.
Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Kahama, Mataruma Kaniki Maganyala, amesema kupata hati safi kumeongeza ari na kujiamini kwa viongozi na watumishi kuendelea kusimamia vizuri rasilimali za umma na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.





















Social Plugin