MDOGO WA DADA ALIYEUAWA ASIMULIA MGOGORO ULIVYOKUWA MWANZO MWISHO...UCHAWI WAHUSISHWA


Swalha enzi za uhai wake 


Picha ya Marehemu Swalha akiwa na mume wake

Mwanaume aitwaye Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28)  mkazi wa Kirumba jijini Mwanza usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022 amekutwa amejiua.


Wanandoa hao walifunga pingu za maisha Disemba 30, 2021.  


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Mairi Makori amethibitisha kujiua kwa Said Oswayo ambaye alikuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake na kwamba mwili wake umekutwa ndani ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza ukiwa na majeraha ya risasi kichwani.


Kamanda Makori amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtu huyo ndiye mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake.

Mdogo wa marehemu mwenye umri wa miaka 15 amesema kabla ya tukio hilo lililotokea usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022 marehemu dada yake na mume wake (shemeji) Said Oswayo walikuwa na ugomvi huku sauti za majibizano zikisikika kutoka chumbani na baadaye walibaini mwili wa dada yake ukiwa kitandani ukivuja damu.


“Mimi na House girl wetu tulikuwa tukiandaa chakula cha usiku. Tuliwasikia dada na shemeji wakizozana kwa muda wa takribani nusu saa ndipo tukasikia milio ya kwanza ya risasi. Nilikimbilia chumbani kwao na kubisha hodi lakini hakukuwa na jibu nikaamua kuondoka. Muda mfupi baada ya milio ya kwanza ya risasi, kulisikika milio mingine na niliporejea tena kugonga mara ya pili mlango wa chumbani,shemeji alitoka na kuniambia kuwa hakuna tatizo niendelee tu shughuli zangu ila akasema wana mkwaruzano  kidogo kutokana na dada yangu kutopokea simu yake zaidi ya mara 37",ameeleza mtoto huyo.


Mama mzazi wa mwanamke aliyefahamika kwa jina la Swalha ambaye ameuawa kwa kupigwa risasi saba kichwani na mume wake kwa sababu ya wivu wa mapenzi amesimulia mkasa mzima kilichopelekea kifo cha mwanaye.


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huko Jijini Mwanza na ndoa yao ilidumu kwa muda wa miezi mitano.


Zaidi tazama hapa kwenye video Mama wa Swalha akizungumzia zaidi.

CHANZO:EATV


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post