SERIKALI YA TANZANIA YATAKIWA KUITAMBUA SIKU YA MFANYAKAZI WA NYUMBANI


Serikali ya Tanzania imehimizwa kuridhia mkataba wa shirika la kazi duniani (ILO) namba 189 uliosainiwa Juni 16, 2011 kwa lengo la kuhimiza maslahi na kazi zenye staha kwa
wafanyakazi wa nyumbani duniani.

Kwa mantiki hiyo, nchi zilizoridhia mkataba huo zinaingia kwenye utekelezaji wa maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani duniani na hivyo kutoa fursa ya kuihamasisha
jamii kulinda na kuheshimu nafasi ya mfanyakazi huyo muhimu katika jamii.

Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) lenye makazi yake jijini Mwanza, limeadhimisha maadhimisho ya Siku
ya Mfanyakazi wa Nyumbani yaliyofanyika katika viunga vya Kishimba Jumapili Juni 16, 2019.

Akizungumzia maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa shirika hilo, Angel Benedicto alisema ni wakati mwafaka sasa Serikali ya Tanzania kuridhia mkataba huo ili kuitambua rasmi Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani Duniani na kuiadhimisha ili kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kulinda maslahi ya kada hiyo tofauti na ilivyo kwa baadhi
ya maeneo ambapo bado wafanyakazi wa nyumbani wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo maslahi duni.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakiingia kwenye viunga vya Kishimba kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani Duniani 2019.
Wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakionyesha jumbe mbalimbali kupitia mabango.
Wageni waalikwa meza kuu wakisoma jumbe mbalimbali kupitia mabango ya wafanyakazi wa nyumbaji jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza walihimiza kulipwa ujira wao kwa wakati na kwa mujibu wa sheria ambapo kima cha chini ni shilingi elfu 40 kwa mwezi.
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani wakifuatilia maadhimisho hayo.
Jamii inahimizwa kutowaajiri watoto kufanya kazi za nyumbani na badala yake kuwapa fursa ya kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Baadhi ya wazazi na walezi (waajiri) wa watoto wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa), Angel Benedicto akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani yaliyoandaliwa na shirika hilo jijini Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post