WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AKUTANA NA WAWEKEZAJI TOKA UTURUKI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akizungumza na ujumbe wa wafanyabiashara toka nchini Uturuki. Pembeni yake ni Balozi wa Uturuki nchini Mhe Ali Davutaglu
Wafanyabiashara wakimsikiliza kwa makini akiwaeleza kuhusu faida za kuwekeza nchini
Balozi wa Uturuki akimkabidhi Waziri wa Viwanda zawadi ya mojawapo ya bidhaa zinazotengenezwa Uturuki kwa niaba ya ujumbe wa wafanyabiashara
Mheshimiwa Innocent Bashungwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara pamoja na balozi wa Uturuki
………………..
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amekutana na ujumbe wa wafanyabiashara toka nchini Uturuki katika ofisi za Kiuo cha Uwekezaji
(TIC).

Ujumbe huo ulioongozwa na balozi wa Uturuki nchini Mheshimiwa Ali Davutaglu ulihusisha wafanyabiashara wa sekta za ujenzi, utalii, chakula na viwanda mbalimbali. Wafanyabiashara hao walielezea sifa ya Tanzania kuwa na amani kama kivutio cha wao kutaka kuwekeza nchini na kusema wangependa kufungua ofisi
itakayokuwa kiungo baina ya wafanyabishara wa Uturuki na wale wa Tanzania.

Mheshimiwa Bashungwa amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba Tanzania ni nchi salama na yenye mazingira rafiki kwa wawekezaji akiahidi kuhakikisha Wizara ya Viwanda na Biashara ikishirikiana kwa ukaribu na taasisi nyingine za Serikali itaharakisha taratibu zote zinazotakiwa ili waanze uwekezaji wao mapema iwezekanavyo.

Pia aliahidi kuwakutanisha na wafanyabiashara wengine nchini ili wapate kufahamiana na kubadilishana ujuzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527