Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAANDISHI WA HABARI 64 WAFUZU KUWANIA TUZO ZA SAMIA KALAMU 2026!, WASHINDI KUPEWA TUZO DESEMBA 5 DAR

Waandishi wa habari 64 kutoka vyombo vya habari 11 wamefanikiwa kuingia hatua ya mwisho ya kuwania Tuzo za Uandishi wa Habari za Maendeleo (Samia Kalamu Awards 2026), zinazolenga kutambua na kuenzi mchango wa wanahabari katika kuibua, kuandika na kusambaza habari zinazochochea maendeleo ya jamii na taifa.

Hatua hiyo imetangazwa Novemba 17, 2026, na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) pamoja na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa jijini Dar es Salaam.

Washiriki hao wamefuzu kuwania tuzo katika vipengele mbalimbali, vikiwemo Tuzo za Kisekta, Tuzo kwa Vyombo vya Habari na Tuzo Maalumu za Kitaifa.

Washindi watakaopatikana wanatarajiwa kukabidhiwa tuzo zao katika hafla kubwa itakayofanyika Desemba 5, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com