ALICHOPOST KIBONDE MTANDAONI KABLA YA KIFO CHAKE... INASIKITISHA SANA

Kibonde na mkewe enzi za uhai wao

Ikiwa ni masaa machache tangu mtangazaji pendwa wa Clouds FM, Ephraim Samson Kibonde kufariki dunia, imeonekana kama moyoni mwake alimkumbuka sana mke wake ambaye kwa sasa ni marehemu.

Kibonde alituthibitishia hilo Machi 3,2019 kupitia ukurasa wake wa instagram, baada ya kumpost picha ya marehemu mke wake, siku tatu nyuma kabla ya kufariki dunia, bila kuandika ujumbe wowote.
Kibonde alifiwa na mkewe Julai 2018, kitu ambacho mwenyewe alikiri kuwa ndio tukio kubwa lililoumiza moyo kwenye muda wote wa maishani mwake, kutokana na jinsi alivyokuwa karibu na mke wake, na kuwa kama rafiki yake kutokana na upendo ambao alikuwa nao.

Ephraim Kibonde ameacha watoto watatu, Junior,Hilda na Ilaria, ambao kwa sasa watakuwa wamebaki yatima kwa kumpoteza na baba yao pia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527