WAZIRI KALEMANI AIVUNJA BODI YA WAKURUGENZI YA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)


Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma baada ya leo kufikia uamuzi wa kuivunja bodi ya wakurugenzi ya wakala wa Nishati vijijini (REA)

..........................

Na.Alex Sonna,Dodoma.

Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani leo (Novemba 12.2018) amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijiji REA kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wake.

Waziri Kalemani amewaambia waandishi wa habari leo jijini hapa kuwa bodi hiyo iliundwa mwaka 2017 kwa mujibu wa sheria ya wakala vijijini No.8 ya mwaka 2005.


“Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu 9 (3)(b) cha sheria No. 8 ya nishati vijijini ya 2005 nimeamua kuivunja bodi kwa kutengua uteuzi wa mwenyejuti pamoja na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya wakala wa nishati vijijini kuanzia leo tarehe 12 novemba 2018″amesema Kalemani.

Aidha amesema kuwa bodi nyingine itaundwa baadae kwa mujibu wa sheria ya nishati vijijini ya mwaka 2005 Bodi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mwenyekiti wake Gigion Kaunda ilidumu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya mwaka jana.

Dk, Kalemani amesema kuwa Bodi mpya itaundwa badaye kwa mujibu wa sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005.

Wajumbe wa Bodi ambao wametenguliwa ni pamoja na Mhandisi Innoceent Lwogwa,Happiness Mhina,Stella Mandago, Scholastica Jullu,Amina Chinja,Teobard Sabi na Michael Nyagoga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527