UZINDUZI WA ALBAMU YA JERUSALEM BAND WAFANA JIJINI MWANZA


Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa albamu ya kwaya ya "Jerusalem Band" kutoka Kanisa la EAGT Kiloleli lililopo Manispaa ya Ilemela chini ya Mchungaji Mwl. Dkt. Jacob Mutashi (kushoto). Uzinduzi huo ulifanyika jana Novemba 11, 2018 katika ukumbi wa Belmont Fairmont Hotel Jijini Mwanza.
Askofu Eugen Mulisa (wa kwanza kushoto) kutoka kanisa la HHC Alive la Jijini Mwanza akifungua hafla hiyo kwa maombi.
Baadhi ya wanakwaya ya "Jerusalem Band" akiwemo mama mchungaji Dkt. Jacob Mutashi (wa pili kulia).
Miongoni mwa wanakwaya ya "Jerusalem Band" wakipanda jukwaani kusoma risala ya uzinduzi huo.
Mwanafamilia ya "Jerusalem Band", Moses Mutashi akitoa salamu za shukrani kwenye hafla hiyo.
Moses Mutashi (kushoto) akiteta jambo na mshereheshaji Emmanuel Mgaya a.ka. Masanja Mkandamizaji (kulia).

Na George Binagi-GB Pazzo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527