Na Stela
Paul,Shinyanga
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Kati imefanya ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji ya walipa kodi katika mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuendelea kuimarisha na kuboresha mahusiano baina ya mamlaka hiyo na wateja wake.
Ziara hiyo imefanyika leo Oktoba 9, 2026 ikiongozwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Maro, ambapo viongozi hao wamesikiliza na kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili walipa kodi hao
Akizungumza mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Jambo Food Product Meneja Maro amebainisha kuwa ziara hiyo imekuwa sehemu muhimu ya kujifunza, namna walipa kodi wanavyotekeleza shughuli zao za uzalishaji na kwamba itakuwa chachu ya maendeleo hususani kwenye eneo la usimamizi wa mapato
" Imekuwa ni fursa nzuri ya kuona uhalisia wa shughuli zinazoendelea na imetupa fursa ya kujifunza tunavyoshirikiana na nyie katika usimamizi wa kodi ili tuwe tunatambua nini kinaendelea" amesema Meneja Maro
Aidha, ameongeza kuwa moja kati ya jukumu watakaloendelea kulitekeleza ni kuhakikisha wanashirikiana na wateja wao ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili pamoja na kutoa huduma bora kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla
"Tunaahidi kuwa ziara hii itakuwa ni sehemu ya sisi kushirikiana na nyie na kutatua changamoto zinapojitokeza na Kutoa wepesi katika huduma" ameongeza Maro

Sambamba na ziara hiyo, awali viongozi hao wametoa zawadi kwa baadhi ya walipa kodi wa Mkoa wa Shinyanga kama sehemu ya kutambua mchango wao katika kukuza maendeleo ya uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla
Walipa kodi hao ni pamoja na kampuni ya Jambo Group Limited, Gilitu Enterprises Limited, Gaki Investment Company Limited na Fresho Investment Company Limited
Ikumbukwe kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 Mamlaka ya Mapato Tanzania Kanda ya Kati inayojumuisha Mkoa wa Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Kigoma, Katavi na mkoa wa kikodi Kahama, ilivuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya asilimia 100 na kufanikiwa kupata hati safi.
Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo Mkoa wa Shinyanga imesherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo imeanza Oktoba 5 na imehitimishwa leo Oktoba 9, 2026 kwa kuwafikia walipa kodi mbalimbali.
TAZAMA PICHA HAPA👇👇👇👇👇















































Social Plugin