Na Sheila Ahmadi, Geita
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameipongeza NSSF kwa mafanikio iliyoyapata katika kuimarisha huduma za hifadhi ya jamii na kusisitiza umuhimu wa kuongeza idadi ya wanachama nchini.
Sangu amesema utii wa sheria kwa waajiri, hususan katika kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, ni muhimu katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata stahiki zao kwa wakati.
Pia makampuni makubwa ya madini, ikiwemo Geita Gold Mining Limited (GGML), akisisitiza kuwa waajiri wana wajibu wa kuhakikisha michango ya wafanyakazi inawasilishwa kwa wakati kwa mujibu wa sheria.
Aidha, Sangu ameipongeza Serikali ya Mkoa wa Geita kwa kutoa fursa kwa NSSF kushiriki katika maonyesho hayo, akisema ushiriki huo ni muhimu katika kuwafikia wananchi na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii.
Ameutaka uongozi wa NSSF kuendeleza kasi ya kuongeza wanachama, akibainisha kuwa Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita amepewa lengo la kusajili wanachama wapya 5,000 ndani ya mwaka huu.
Vilevile waziri Sangu, tayari zaidi ya nusu ya lengo hilo limefikiwa, hivyo amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha wanachama waliobaki wanasajiliwa ili lengo hilo litimie kabla ya mwaka huu kumalizika.
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa NSSF, Lulu Mengele, amesema thamani ya mfuko huo imefikia Sh trilioni 11.5, hatua inayoonyesha kuendelea kukua kwa uwezo wa mfuko katika kutekeleza majukumu yake.

Social Plugin