Singida, Tanzania
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndg. Rabia Abdalla Hamid, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kutimiza wajibu wake wa kushughulikia changamoto na matatizo yanayowakabili wananchi kwa vitendo.
Rabia amesema hayo leo, Septemba 24, 2026, alipokuwa katika ziara mkoani Singida, ambapo amepokelewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Singida na baadaye kutembelea Jengo la Wazazi katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, mjini Singida.
Akiwa hospitalini hapo, Rabia amejionea utekelezaji wa Ilani ya CCM, hususan katika utoaji wa huduma za afya kwa wanawake na watoto.
Katika ziara hiyo, pia ametembelea vikundi vya wajasiriamali na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili, huku akitoa maelekezo ya namna ya kuzitatua.
Aidha, amekutana na kusikiliza maoni na changamoto za makundi mbalimbali ya kijamii, yakiwemo viongozi wa dini, wazee, machifu, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, mafundi gereji, mafundi ujenzi, wanamichezo, wanafunzi wa vyuo, walimu, machinga, mawinga, mama na baba lishe, watu wenye mahitaji maalum, wajane na wagane, vyama vya ushirika pamoja na maafisa usafirishaji.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Rabia amesema CCM itaendelea kuwa karibu na wananchi na kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi kwa kuzingatia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030.
“CCM itaendelea kutimiza wajibu wake kikamilifu wa kushughulikia changamoto pamoja na matatizo ya wananchi, kama ilivyoahidi katika Ilani yake ya 2025–2030. Hivyo, wananchi waendelee kuiamini CCM kwani ipo kazini kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi wa moja kwa moja,” amesema Rabia.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Social Plugin