Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LINDI YAJIPANGA KUVUTIA WAWEKEZAJI KUPITIA SEKTA YA MADINI RC - MALIMA



Na Sheila Ahmadi, Ruangwa

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Adam Malima amewataka wadau wa sekta ya madini kutumia fursa zilizopo katika sekta hiyo ili kuongeza uzalishaji, ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla.

sekta ya madini ina fursa kubwa za uwekezaji na kwamba kongamano pamoja na maonesho ya madini yanatoa nafasi kwa wadau kubadilishana uzoefu, ujuzi na taarifa zinazoweza kusaidia kuendeleza sekta hiyo.

Akizungumza kwenye Maonyesho ya Madini Mkuu wa Mkoa wa lindi Mhe. Adam Kighoma Malima Mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo Mkuu wa mkoa huo amesema kuwa maonesho hayo hayapaswi kuonekana kama tukio la kawaida, bali yanapaswa kujengwa na kuendelezwa hadi kufikia hatua ya kuvutia washiriki na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema baadhi ya maonesho ya madini nchini yameanza kwa kiwango kidogo lakini baadaye yamekua na kuingia katika ratiba za kimataifa, hivyo Mkoa wa Lindi unapaswa kutumia fursa hiyo kujenga maonesho yenye hadhi na mvuto kwa wawekezaji.

Maonesho haya si jambo la ‘show’ tu. Tunapaswa kuhakikisha yanaendelea kukua na kufikia hatua ambayo makampuni makubwa ya madini duniani yanaweka katika ratiba zao na kuyafanya kuwa sehemu ya kukutana, kubadilishana taarifa na kujenga mitandao ya kibiashara.

" uwepo wa wadau mbalimbali katika kongamano hilo ni fursa muhimu ya kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya madini na kutafuta suluhu zitakazowezesha sekta hiyo kukua zaidi" Amesema Mkuu wa Mkoa Malima".

Sanjari na hilo Mkuu wa mkoa Malima ameongeza kuwa Lindi ina fursa kubwa katika sekta ya madini ambazo zinahitaji kutangazwa na kutumiwa ipasavyo ili kuvutia wawekezaji na kuongeza manufaa kwa wananchi.

Hata hivyo neno fursa linapaswa kutafsiriwa kama nafasi inayojitokeza kwa wakati na katika eneo maalumu, hivyo wadau wanapaswa kuwa tayari kuitumia nafasi hiyo kwa ajili ya maendeleo.

Aidha amewataka wadau wa sekta ya madini kuendelea kushirikiana, kubadilishana taarifa na kujenga mitandao ya kibiashara ili kuhakikisha rasilimali zilizopo Mkoa wa Lindi zinatumika kuongeza thamani na manufaa kwa wananchi.

Kongamano hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini, likiwa na lengo la kujadili fursa, changamoto na namna ya kuimarisha ushirikiano katika kukuza sekta hiyo








.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com