Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BRELA YATOA ELIMU YA ULINZI WA UBUNIFU NA ALAMA ZA BIASHARA GEITA




Na Sheila Ahmadi, Geita

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wafanyabiashara, wachimbaji madini, wajasiriamali na wavumbuzi mkoani Geita kutumia fursa ya maonyesho yanayoendelea mkoani humo kupata elimu na kusajili alama za biashara pamoja na kulinda ubunifu wao.

Akizungumza katika maonyesho hayo, Afisa kutoka BRELA, Athumani Salum Makuka, amesema BRELA imeshiriki maonyesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo, ikiwemo usajili wa kampuni, majina ya biashara, utoaji wa leseni na ulinzi wa ubunifu.

moja ya maeneo muhimu wanayoyahamasisha wananchi ni usajili wa alama za biashara na huduma (trademarks) ambazo hutumika kutambulisha bidhaa au huduma ya mfanyabiashara na kuilinda dhidi ya kutumiwa na mtu mwingine bila ruhusa.

“Tunashughulika zaidi na alama za biashara ambazo kwa Kiingereza zinaitwa trademark. Watu wengine huzita nembo au brand, lakini jina rasmi ni alama za biashara au huduma,” amesema Makuka.

Aidha BRELA inatoa ulinzi wa kisheria kwa wavumbuzi kupitia usajili wa patent, ambao unahusu uvumbuzi wa kitu kipya chenye uwezo wa kutatua changamoto au kuboresha maisha ya jamii.

Makuka amesema kuna tofauti kati ya ugunduzi na uvumbuzi, akieleza kuwa ugunduzi ni kugundua kitu ambacho tayari kipo, wakati uvumbuzi unahusisha ubunifu wa kitu au mfumo mpya unaolenga kutatua tatizo lililopo.

Vilevile fursa hiyo ni muhimu kwa vijana wa mikoa ya Geita na Mwanza ambao wanaweza kubuni teknolojia na mitambo midogo itakayosaidia wachimbaji wadogo kuongeza ufanisi katika shughuli zao.

Katika hatua nyingine mikoa ya Geita na Mwanza inaweza kuwa na vijana wenye ubunifu wa kubuni mitambo midogo ya kuwasaidia wachimbaji wadogo katika uchimbaji na uchangaji wa madini. Kama wavumbuzi hao wapo, sisi tunawasaidia kupata ulinzi wa ubunifu wao,” amesema Makuka

Ameongeza kuwa baada ya mvumbuzi kupata ulinzi wa uvumbuzi wake, anaweza pia kusajili alama au chapa itakayotambulisha bidhaa yake, hatua ambayo husaidia kulinda utambulisho wa biashara hiyo.

katika sekta ya madini, baadhi ya wafanyabiashara wanaotoa huduma za uchimbaji na ushauri wanaweza kuangalia madaraja yanayohusiana na huduma hizo, huku wanaohusika na bidhaa nyingine kama kemikali, vipodozi na tiba wakiangalia madaraja yanayolingana na shughuli zao.

Hivyo watoa huduma katika sekta ya habari na mawasiliano nao wanaweza kusajili alama zao katika madaraja yanayohusiana na huduma wanazotoa, ikiwemo daraja la 38 na 41.

Makuka amewataka wananchi kutumia huduma zinazotolewa na BRELA katika maonyesho hayo, akisema wananchi wanaweza kupata elimu na kusaidiwa kufanya usajili bila kulipia gharama za uendeshaji wa huduma hiyo.

Kupitia usajili wa alama za biashara ni muhimu kwa kuwa unamsaidia mfanyabiashara kulinda utambulisho wa bidhaa au huduma yake na kujenga msingi wa biashara yenye utambulisho unaotambulika kisheria.

Nitoe wito kwa wananchi, hususani wafanyabiashara, wachimbaji, wajasiriamali na wavumbuzi wanaoshiriki maonyesho hayo, kutumia fursa hiyo kupata elimu na kuanza taratibu za kusajili na kulinda biashara pamoja na ubunifu wao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com