Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VETA YATENGENEZA MAVAZI YA USALAMA KWA WACHIMBAJI WA MADINI



Na Sheila Ahmadi, Geita

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kimeanza kutengeneza mavazi maalumu ya usalama kwa ajili ya wafanyakazi katika sekta ya madini na maeneo mengine ya kazi, hatua inayolenga kuongeza usalama kwa wafanyakazi pamoja na kuwapa wanafunzi ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.

Akizungumza katika Maonesho ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Mkufunzi kutoka fani ya ushonaji nguo chuo cha veta Mwanza Veronica Mpinda VETA amesema kuwa ushiriki wa chuo hicho katika maonesho hayo unalenga kuonyesha bidhaa zinazotengenezwa na wanafunzi pamoja na kutafuta masoko na oda kutoka kwa wadau mbalimbali, hususan wanaofanya shughuli za uchimbaji madini.

Kupitia Mavazi hayo yanatumika katika mazingira mbalimbali ya kazi, ikiwemo migodini, huku uzalishaji wake ukitoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kupata uzoefu unaoweza kuwasaidia baada ya kumaliza mafunzo yao.

“Tumekuja hapa kwa ajili ya kuonyesha bidhaa tunazotengeneza, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wetu pamoja na kutafuta soko. Tunaamini tunaweza kupata oda kutoka kwa watu wanaofanya kazi katika sekta ya madini kwa ajili ya kutengeneza mavazi mbalimbali ya usalama sehemu za kazi,” alisema Mpinda

mafunzo hayo yana nafasi kubwa katika kuwaandaa wanafunzi kujiajiri au kuajiriwa, kwa kuwa wanapofundishwa kutengeneza bidhaa zinazohitajika sokoni, wanapata wigo mpana wa kutumia ujuzi wao baada ya kuhitimu.

Hata hivyo VETA imeamua kupeleka bidhaa hizo kwenye maonesho ili kuwaonyesha wananchi na wadau kuwa bidhaa hizo zinaweza kutengenezwa nchini, badala ya kutegemea bidhaa kutoka nje.

kupitia maonesho hayo, chuo kinatarajia kupata wateja na oda mbalimbali ambazo zitaongeza uzalishaji na kuwapa wanafunzi fursa zaidi za kujifunza kwa vitendo.

Vilevile upekee wa mavazi hayo ni matumizi ya vitambaa vizito vinavyoweza kudumu kwa muda mrefu na kutumika mara kadhaa baada ya kufuliwa, tofauti na baadhi ya mavazi mepesi ambayo yanaweza kuchakaa kwa haraka.

“Vitambaa tunavyotumia hapa ni vizito na vina uwezo wa kudumu. Mtu anaweza kuvaa, kikachafuliwa, akafulia na akaendelea kutumia tena. Hiyo ni tofauti na baadhi ya nguo zinazotengenezwa kwa vitambaa vyepesi ambavyo vinaweza kutumika mara moja na visiwe na uimara unaohitajika,” alisema.

Sanjari na hayo uwepo wa bidhaa hizo katika maonesho unalenga pia kuwaonyesha wadau uwezo wa ndani katika kutengeneza vifaa na mavazi yanayokidhi mahitaji ya sekta ya madini, huku wanafunzi wakipata nafasi ya kujifunza na kujiandaa zaidi kwa soko la ajira.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com