Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIMARISHA ULINZI WA BAHARINI, YAHARAKISHA UANZAJI WA KITUO CHA KITAIFA CHA OPARESHENI WAZIRI NCHEMBA




Na Sheila Ahmadi, Dar es salaam


Serikali imechukua hatua mpya katika kuimarisha usalama wa baharini na uratibu wa taasisi za ulinzi baada ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, kuagiza Kituo cha Kitaifa cha Pamoja cha Oparesheni kianze kufanya kazi ndani ya siku 14.

Akizungumza jijini Dar es salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa boti hizo mbili za doria na uokozi aina ya PB Sailfish 02 na PB Sailfish Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu nchemba alisema wizara na taasisi zote zinazohusika zinapaswa kupeleka wawakilishi wao ndani ya muda huo ili kituo hicho kianze kutekeleza majukumu yake bila kuchelewa.

kuanza kwa kituo hicho kutaimarisha ushirikiano wa taasisi za Serikali katika kulinda mipaka ya bahari, kupambana na uhalifu na kuhakikisha rasilimali za uchumi wa bluu zinalindwa ipasavyo.

"Nitoe Wito Kwa taasisi zitakazotumia boti hizo kuhakikisha zinatenga fedha za kutosha kwa ajili ya uendeshaji, mafuta na matengenezo ili zifanye kazi kwa ufanisi wakati wote." Amesema Dkt Nchemba

Vilevile uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali unaweza kupoteza tija endapo hakutakuwa na fedha za kuendesha vifaa hivyo, akitolea mfano baadhi ya magari ya wagonjwa yaliyoshindwa kutoa huduma kwa wakati kutokana na changamoto za uendeshaji.
Aidha, alisema boti hizo zitasaidia kuongeza usalama katika Bahari ya Hindi na eneo la Bandari ya Dar es Salaam, lango muhimu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani za Afrika Mashariki na SADC.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, alisema boti hizo zenye thamani ya dola za Marekani milioni 1.6 zimetengenezwa nchini Japan kwa viwango vya kimataifa na zimekaguliwa na wataalamu wa Serikali kabla ya kukabidhiwa.

Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mikami Yoichi, alisema ushirikiano kati ya Tanzania na Japan utaendelea kuunga mkono juhudi za kuimarisha usalama wa baharini na kulinda maisha pamoja na shughuli za kiuchumi zinazotegemea bahari.












Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com