Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026. Picha na Kadama Malunde
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga
Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga imewataka vijana wake kuendelea kulinda amani, kujiepusha na mijadala ya matusi kwenye mitandao ya kijamii na badala yake kujikita katika kueleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kama njia bora ya kujibu hoja za wapinzani.
Wito huo umetolewa leo Juni 24, 2026 na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo amesisitiza kuwa vijana wa CCM wanapaswa kuwa mabalozi wa amani, maendeleo na mshikamano wa taifa.
Werema amesema vijana wa UVCCM, ambao ni sehemu ya chama kinachoiongoza serikali, wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia wananchi bila ubaguzi, kusikiliza changamoto zao na kuzifikisha katika mamlaka husika, sambamba na kuhamasisha vijana kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotolewa na serikali.
"Vijana wa Mkoa wa Shinyanga tusijibu matusi mtandaoni. Tueleze mambo makubwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tuwaambie vijana kuwa serikali haijalala. Wapinzani wanajaribu kuharibu taswira ya serikali kwa kutumia matusi badala ya hoja, lakini sisi tuwaeleze wananchi kuhusu fursa zilizopo na maendeleo yanayoendelea kutekelezwa," amesema Werema.
Ametaja baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Shinyanga kuwa ni pamoja na Mradi wa Umeme wa Jua Kishapu, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Shinyanga pamoja na miradi mingine katika sekta mbalimbali, akisisitiza kuwa hayo ndiyo yanapaswa kuwa ajenda kuu za vijana wa CCM wanapozungumza na wananchi.
"Tusitumie muda mwingi kuhangaika na matusi. Tuwajibu wapinzani kwa vitendo, kwa kueleza mafanikio ya serikali na kwa kusikiliza pamoja na kutatua kero za wananchi," ameongeza.
Werema amesema UVCCM itaendelea kuwa nguzo ya kulinda amani, utulivu na mshikamano wa taifa huku ikiunga mkono juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
"Tupo tayari kuipigania serikali dhidi ya wanaotaka kuharibu taswira ya nchi yetu. Vijana tutaendelea kuhubiri amani na hatutakuwa tayari kushiriki vitendo vya kuvuruga utulivu wa nchi. Ni jukumu letu kulinda serikali, kulinda taifa letu na kushirikiana kutatua changamoto za wananchi. Amani tuliyonayo lazima tuilinde," amesema.
Katika hatua nyingine, amesisitiza kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila amani na kuwataka vijana kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuilinda.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga.
"Naomba tutunze amani ya nchi. Hatuwezi kufanya maendeleo bila amani. Tuwaambie wale wenye nia ya kuvuruga amani kuwa sisi tunahitaji amani. Sisi vijana hatuna muda wa kuvuruga amani, bali tuna jukumu la kushiriki katika maendeleo ya taifa," amesema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amesema UVCCM ni tanuru la kuandaa viongozi wa taifa na nguzo muhimu katika kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi.
Mhita amesema vijana wanapaswa kutumia nafasi waliyopewa ndani ya jumuiya hiyo kujifunza misingi ya uongozi, uzalendo na uwajibikaji ili waweze kuwa viongozi bora wa kesho.
"Jumuiya ya Vijana ni tanuru la kuoka viongozi. Hapa ndipo viongozi wengi wanapoandaliwa na kujengwa. UVCCM ni hazina ya viongozi wa taifa letu," amesema Mhita.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kuwawezesha vijana kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa fursa mbalimbali za kiuchumi.
"Dkt. Samia ni kiongozi anayewapenda vijana. Ni lazima vijana wawe na nidhamu. UVCCM ni jeshi la CCM ambalo lipo tayari kukitetea chama na kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema.
Mhita amesema Mkoa wa Shinyanga umeendelea kunufaika na uwekezaji mkubwa wa serikali katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia ambapo zaidi ya shilingi trilioni 1.7 zimeelekezwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Samia, Mkoa wa Shinyanga umepokea zaidi ya shilingi trilioni 1.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na imeendelea kuboresha huduma kwa wananchi," amesema.
Aidha, amewataka viongozi wa UVCCM na vijana kwa ujumla kuwa mabalozi wa maendeleo kwa kuwaelimisha wenzao kuhusu fursa zinazotolewa na serikali, hususan mikopo ya vijana inayotolewa kupitia halmashauri.
"Vijana waendelee kufuatilia na kutumia fursa zilizopo. Serikali imetoa fursa nyingi kwa vijana kuanzia ngazi ya halmashauri. Ninyi ndiyo wasemaji na watetezi wa vijana, waelekezeni namna ya kunufaika na fursa hizo na wahamasisheni kuchukua mikopo na kuirejesha kwa wakati," amesema.
Mhita pia amewapongeza vijana wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwa nidhamu, ushiriki wao katika ziara mbalimbali za chama na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, akisema juhudi hizo zimeendelea kuimarisha chama na kuongeza idadi ya wanachama wapya.
"Nawapongeza vijana wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwa nidhamu yenu, kwa kufanya ziara na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Mnaifanya CCM iendelee kuwa hai na kuendelea kupata wanachama wapya," amesema.
Naye Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo, amewataka vijana wa UVCCM kuendelea kukijenga chama kwa umoja, mshikamano na nidhamu huku akiwahimiza kujiepusha na makundi yasiyo na tija ambayo yanaweza kudhoofisha nguvu na umoja wa chama.
Batimayo amesema vijana wanapaswa kuwa na maono makubwa ya uongozi na kujiandaa kuwa viongozi wa baadaye kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kutanguliza maslahi ya chama na wananchi.
"Naomba tuepuke makundi ndani ya chama. Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake, tuwaunge mkono viongozi wetu na tuendelee kuimarisha mshikamano ndani ya CCM," amesema Batimayo.
Ameongeza kuwa umoja, nidhamu na uwajibikaji vitasaidia chama kuendelea kuwa imara na kuandaa viongozi bora watakaoendeleza dhamana ya kuwatumikia wananchi siku zijazo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benson Werema, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026. Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Salama Mhampi akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga kilichofanyika leo Juni 24, 2026.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo, akizungumza katika kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Shinyanga.

Social Plugin