Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari–Maelezo, Zamaradi Kawawa akizungumza kwenye kikao cha wadau wa sekta ya habari chenye lengo la kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kuhamasisha amani, utulivu, umoja wa kitaifa na maridhiano nchini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blogDkt. Egbert Mkoko kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha mada kuhusu uandishi wa habari unaojenga taifa badala ya kubomoa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Idhibati ya Waandishi wa Habari, Patrick Kipangula akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuhamasisha amani na maridhiano

Mhandisi Andrew Kisaka kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akiwasilisha mada kuhusu utangazaji wakati wa migogoro.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanablogu Tanzania ( Tanzania Bloggers Network - TBN), Beda Msimbe akizungumza kwenye kikao cha wadau wa sekta ya habari chenye lengo la kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kuhamasisha amani, utulivu, umoja wa kitaifa na maridhiano nchini.Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime akizungumza kwenye kikao cha wadau wa sekta ya habari chenye lengo la kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kuhamasisha amani, utulivu, umoja wa kitaifa na maridhiano nchini.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari – Maelezo imeendesha kikao cha wadau wa sekta ya habari kwa lengo la kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kuhamasisha amani, utulivu, umoja wa kitaifa na maridhiano nchini.
Kikao hicho kimefanyika Aprili 17, 2026 katika ukumbi wa PSSSF Commercial Complex jijini Dar es Salaam, na kuongozwa na Zamaradi Kawawa, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – Maelezo, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kawawa amesema kuwa lengo kuu ni kuwajengea uelewa wadau wa sekta ya habari kuhusu wajibu wao katika kulinda na kuimarisha amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa kupitia kazi zao za kila siku.
Kawawa amewataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya taaluma yao hasa katika vipindi vya changamoto au migogoro, akisisitiza umuhimu wa kuandika habari zenye kujenga mshikamano wa kitaifa.
“Wakati wa mgogoro sisi waandishi wa habari tunatakiwa kuandika habari za kujenga. Tunapaswa kuhamasisha amani, utulivu, umoja wa kitaifa na maridhiano nchini. Hakikisheni mnaandika habari zinazowaunganisha Watanzania, si zinazobomoa taifa,” amesema Kawawa.
Washiriki wa kikao hicho wamejumuisha viongozi na wanachama kutoka Tanzania Bloggers Network (Mtandao wa Wanablogu Tanzania - TBN), JUMIKITA (Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania) pamoja na TADIO (Mtandao wa Redio za Kijamii Tanzania).
Katika kikao hicho, mada mbalimbali ziliwasilishwa na wataalamu kutoka taasisi tofauti. Miongoni mwa mada hizo ni pamoja na wajibu wa waandishi wa habari katika kuhamasisha amani na maridhiano, mada iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Idhibati ya Waandishi wa Habari, Patrick Kipangula.
Aidha, Dkt. Egbert Mkoko kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amewasilisha mada kuhusu uandishi wa habari unaojenga taifa badala ya kubomoa, huku Mhandisi Andrew Kisaka kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akiwasilisha mada kuhusu utangazaji wakati wa migogoro.





























































































Social Plugin