Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Idhibati ya Waandishi wa Habari, Patrick Kipangula akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuhamasisha amani na maridhiano

Na Mwandishi Wetu
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema uandishi wa habari usiozingatia maadili unaweza kuhatarisha umoja wa kitaifa, amani na utulivu wa jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari ambao ni wanachama wa JUMIKITA, TADIO na TBN, leo Ijumaa Aprili 17, 2026 jijini Dar es Salaam, Kipangula alisema waandishi wa habari wanapaswa kutambua uzito wa nafasi yao katika jamii, hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, ambapo taarifa wanazozitoa zina athari kubwa kwa mwenendo wa jamii.
Alifafanua kuwa amani ni hali ya kutokuwepo kwa migogoro au vurugu, huku utulivu ukimaanisha usalama na uhakika wa maisha ya wananchi bila hofu, akibainisha kuwa hali hizi mbili haziwezi kudumu bila uwepo wa umoja wa kitaifa unaojengwa juu ya mshikamano wa wananchi bila kujali tofauti zao.
“Pale ambapo uandishi hauzingatii maadili, unaweza kuchochea migawanyiko, kupotosha ukweli na hatimaye kuvuruga mshikamano wa kitaifa. Hivyo, ni muhimu kwa waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uwajibikaji,” alisema Kipangula.
Alibainisha kuwa waandishi wa habari wana wajibu wa msingi wa kukusanya, kuchakata na kusambaza taarifa sahihi, pamoja na kusaidia kuunda mitazamo ya wananchi kwa njia inayochangia maridhiano na maendeleo ya jamii.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Taaluma ya Uandishi wa Habari, akibainisha kuwa maadili hayo yanahimiza ukweli, usawa, uwazi na heshima kwa haki za binadamu, mambo ambayo ni msingi wa kulinda amani, kuimarisha utulivu na kukuza umoja wa kitaifa.

Social Plugin