Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VETA KWIMBA YANADI MAFANIKIO NA MIKAKATI YA KUJENGA TANZANIA YENYE MAFUNDI MAHIRI NA WA KUTOSHA



Na Lulu Mbwaga _
Mwanza .

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi - VETA Kwimba imenadi mipango  na kikakati yake  kwenye kufikia malengo iliyojiwekea ya kuwa na Tanzania yenye Mafundi Mahiri na wa kutosha.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa Chuo cha VETA Kwimba ,Elias Msigwa amesema kuwa, VETA Kwimba inajipanga kuhakikisha mambo yafuatayo yanatekelezwa ipasavyo, kuhakikisha watu wenye mahitaji maalumu wananufaika na huduma za VETA ili kuwa na haki sawa na wengine, kutumia vifaa na mashine za kisasa ili kuboresha stadi za ufundi kwa wanafunzi Chuoni hapo , kunufaika na mradi wa kilimo kupitia  teknolojia ili kuendana sambamba ma matumizi ya teknolijia kwenye kilimo na kuongeza tija ya kilimo. 

Msigwa pia ameongeza kuwa, VETA Kwimba wanatekeleza majukumu yao kikamilifu kupitia kauli mbiu  ya kitaifa  ya " Tanzania yenye Mafundi Mahiri na wa kutosha" ili kufikia malengo ya mikakati na maoni ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA.

Msigwa pia amehitaka jamii kuchangamkia fursa za masomo kupitia VETA ili kupata ujuzi wa kuajiriwa au kujiajiri.

" Kwa sasa tunapanga kuongeza muda wa masomo kutoka kuwa na masomo ya asubuhi hadi kwenda kuwa na masomo ya asubuhi na  jioni ili kutoa fursa kwa watu wengine wanaotaka kujiendeleza kupata fursa hizo" amesema Msigwa.

Mkutano huo na Vyombo vya habari umefanyika leo Jijini Mwanza kwa lengo la kueleza mipango na mikakati ya VETA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com