Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewasili Mkoani Arusha Januari 31, 2026 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Mhe. Nchemba anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye Kilele cha tuzo za 'The Serengeti Awards', ikiwa ni ushuhuda wa dhamira ya Tanzania katika kutambua na kuthamini mchango wa wadau, kuenzi ubora na kuendeleza utalii endelevu sambamba na uhifadhi wa maliasili za Tanzania.




Social Plugin